

Lugha Nyingine
China yasema inapenda kuendeleza mradi kinara wa BRI, kuhimiza biashara na uwekezaji na Ethiopia
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed pembezoni mwa Mkutano wa 17 wa Kilele wa BRICS mjini Rio de Janeiro, Brazil, Julai 6, 2025. (Xinhua/Yao Dawei)
RIO DE JANEIRO - China inapenda kushirikiana na Ethiopia kuhimiza maendeleo endelevu ya Reli ya Addis Ababa-Djibouti, mradi kinara wa ushirikiano wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI), na kupanua biashara na uwekezaji wa pande mbili, Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema jana Jumapili mjini Rio De Janeiro, Brazil alipokutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed pembezoni mwa Mkutano wa 17 wa Kilele wa BRICS.
"Tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Ethiopia miaka 55 iliyopita, nchi hizo mbili zimekuwa zikitendeana kwa udhati na kuungana mkono bila kujali hali ya kimataifa inavyobadilika," Li amesema, akiongeza kuwa ushirikiano kati ya pande hizo mbili kwa muda mrefu umekuwa mstari wa mbele katika ushirikiano kati ya China na Afrika.
Li amesema Rais Xi Jinping wa China alituma barua ya pongezi kwa Mkutano wa Mawaziri Waratibu juu ya Utekelezaji wa matokeo yaliyofikiwa kwenye Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) mwezi Juni, akitangaza hatua mpya muhimu kama vile kutekeleza kutoza ushuru-sifuri kwa asilimia 100 za bidhaa zenye kustahiki kutozwa ushuru kutoka nchi 53 za Afrika ambazo zina uhusiano wa kidiplomasia na China.
Li amesema China itachukua hatua hizo mpya kama fursa za kushirikiana na Ethiopia ili kutekeleza kwa pande zote matokeo ya Mkutano wa Kilele wa Beijing wa FOCAC.
Waziri Mkuu huyo wa China ametoa wito wa kuongezwa kwa kina ushirikiano wa mambo yote wa pande mbili na kuufanya uhusiano huo wa pande mbili kuwa mfano wa kuigwa kwa ajili ya kujenga jumuiya ya ya China na Afrika ya hali zote yenye mustakabali wa pamoja kwa zama mpya.
"China, kama inavyofanya wakati wote, itaiunga mkono Ethiopia katika kuchunguza kwa uhuru njia ya maendeleo inayofaa kwa hali yake ya kitaifa, kushirikiana na Ethiopia kuongeza kwa kina ushirikiano katika miundombinu, magari yanayotumia nishati mpya, viwanda vya kijani, biashara ya mtandaoni na akili mnemba, na kuzidisha mawasiliano katika utalii, vijana, elimu na sekta nyingine," Li amesema.
Akisema kuwa China na Ethiopia ni nchi muhimu za Kusini, Li amesema China itaiungana mkono na Ethiopia ili kuimarisha mawasiliano na uratibu ndani ya mifumo ya pande nyingi kama vile Umoja wa Mataifa na BRICS, kuhimiza juhudi kubwa za pande zote kutekeleza mfumo wa kweli wa pande nyingi, kulinda kithabiti utandawazi wa kiuchumi na biashara huria, na kuingiza utulivu na nishati chanya duniani.
Kwa upande wake, Abiy amesema Ethiopia na China ni washirika wa kimkakati wa kuaminika wa hali zote, na kwamba nchi yake inaishukuru kwa dhati China kwa uungaji mkono na msaada wake wa muda mrefu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Ethiopia.
"Ethiopia pia inathamini sana juhudi za China kutekeleza matokeo ya mkutano wa kilele wa FOCAC wa Beijing," ameongeza.
Akiongeza kuwa China ina jukumu muhimu sana katika mambo ya kimataifa, hasa katika harakati ya maendeleo duniani, Abiy amesema Ethiopia inapenda kuzidisha mazungumzo ya ngazi ya juu na China na kuongeza kwa kina hali ya kuaminiana kisiasa.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed pembezoni mwa Mkutano wa 17 wa Kilele wa BRICS mjini Rio de Janeiro, Brazil, Julai 6, 2025. (Xinhua/Yao Dawei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma