Uzuri wa Majira: Joto Kidogo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 07, 2025

Habarini! Mimi ni Sisi, mpenda kusafiri! Leo ni Xiaoshu, au Joto Kidogo, moja kati ya vipindi 24 vya hali ya hewa katika kalenda ya jadi ya China. Jiunge nami katika Eneo linalojiendesha la Makabila ya Wamiao na Wadong la Qiandongnan katika Mkoa wa Guizhou, kusini-magharibi mwa China, eneo linalojivunia uzuri wa kustaajabisha, ili kuepuka joto kali la majira ya joto!

Katika zama za kale, watu walikiita kipindi hiki "Joto Kidogo" kwa sababu ni mwanzo wa hali ya hewa ya joto, ingawa joto lilikuwa bado halijafikia kilele chake. Wakati wa kipindi hiki, kwa kalenda ya kilimo ya China, jua huwaka, mvua huongezeka, harufu nzuri ya yungiyungi hujaa hewani, na matunda huiva. Ni msimu wa ukuaji mkubwa kwa viumbe vyote hai.

Kuwa na nafaka freshi ilikuwa moja ya mila kuu ya China ya kale. Watu hukoboa mpunga freshi uliovunwa wakati wa kipindi cha Joto Kidogo na kula ili kusherehekea mavuno na kuombea hali nzuri ya hewa na mazao mengi katika mwaka unaofuata.

Wakati kipindi cha Joto Kidogo kinapokuja, kipindi cha Sanfu huanza. Vipindi Vya Sanfu, hurejelea vipindi vitatu mfululizo vya siku 10 kulingana na kalenda ya kilimo ya China, ambapo hali ya joto hufikia kilele chake nchini humu. Kwa kuhesabu kutoka solistasi ya majira ya joto, tutaingia vipindi vya Sanfu baada ya Joto Kidogo.

Jambo la kufurahisha, katika nchi za Magharibi, watu walibaini kwamba nyota angavu zaidi katika anga ya usiku, Sirius, huchomoza na jua alfajiri wakati wa joto zaidi katika mwaka. Wanaamini kitendo hiki kilileta joto maradufu, walikiita kipindi hiki "siku za mbwa". Vyote vipindi vya Sanfu vya China na "siku za mbwa" katika nchi za Magharibi vyote vinaonyesha kuwa tamaduni tofauti zimechangia kumbukumbu za majira ya joto kali.

"Mpulizo wa ghafla wa hewa ya joto wakati kipindi cha Joto Kidogo kinapowadia." Katika wakati huu wa maisha kustawi na joto kali, nakutakia mng'ao mkali kama jua la majira ya joto na furahia kila wakati mzuri.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha