China yaadhimisha miaka 88 tangu kuanza kwa vita vya taifa zima dhidi ya uvamizi wa Japan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 08, 2025

Cai Qi, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Katibu wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC, akitoa hotuba kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 88 tangu kuanza kwa vita vya taifa zima dhidi ya uvamizi wa Japan, na kutangaza ufunguzi wa maonyesho yenye kaulimbiu ya "Kwa Ukombozi wa Taifa na Amani Duniani" katika Jumba la Makumbusho ya Vita vya Watu wa China Dhidi ya Uvamizi wa Japan mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 7, 2025. (Xinhua/Shen Hong)

BEIJING - China imefanya hafla mjini Beijing jana Jumatatu kuadhimisha miaka 88 tangu kuanza kwa vita vya taifa zima dhidi ya uvamizi wa Japan ambapo maonyesho yenye kaulimbiu ya "Kwa Ukombozi wa Taifa na Amani Duniani" pia yamezinduliwa ili kuadhimisha miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China dhidi ya Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia dhidi ya Ufashisti.

Vyote hafla na maonyesho hayo yamefanyika katika Jumba la Kumbukumbu ya Vita vya Watu wa China Dhidi ya Uvamizi wa Japan, lililoko karibu na Daraja la Lugou - pia likijulikana kwa jina la Daraja la Marco Polo - ambapo wanajeshi wa Japan walishambulia vikosi vya China Julai 7, 1937.

Cai Qi, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Katibu wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC, alitoa hotuba kwenye hafla hiyo na kutangaza ufunguzi wa maonyesho hayo.

"Wakati askari wa Japan walipofanya Tukio la Daraja la Lugou na kuanzisha uvamizi wao kote nchini China miaka 88 iliyopita, jeshi na watu wa China walisimama katika upinzani, na kuanzisha juhudi za vita vya taifa zima ambavyo vilifungua uwanja mkuu wa vita vya Mashariki katika vita vya dunia dhidi ya ufashisti," amesema Cai.

Cai amesisitiza kuwa CPC ilipigana kwa ujasiri katika mistari ya mbele ya vita hivyo na kuweka mwelekeo wa juhudi za kitaifa, ikihudumu kama nguzo ya taifa zima wakati wote wa vita.

"Wakiwa wameungana kwa nia, watu wa China walipigana kwa dhamira isiyoyumba -- kwa ajili ya kuishi kwa nchi, ustawishaji wa kitaifa, na mambo ya haki ya binadamu wote," Cai amesema, akiongeza kwamba hatimaye walishinda vita na kutoa mchango mkubwa kwenye ushindi katika vita vya dunia dhidi ya ufashisti.

“Maonyesho hayo yanaonesha kwa pande zote mchakato tukufu wa miaka 14 ya vita vigumu vya watu wa China”, amesema Cai, ambaye amesisitiza haja ya kuendeleza moyo wa vita vya watu wa China dhidi ya Uvamizi wa Japan, kuimarisha kujiamini na kusonga mbele ujenzi wa mambo ya kisasa wa China ili kuijenga China kuwa nchi yenye nguvu na ustawi katika nyanja zote.

Vile vile amesisitiza umuhimu wa kutoa mchango mpya na mkubwa zaidi kwa mambo tukufu na adhimu ya amani na maendeleo ya binadamu.

Cai na viongozi wengine waliungana na wawakilishi kutoka sekta mbalimbali kuwasilisha maua kwa wahanga wa vita hivyo. Pia walitembelea maonyesho hayo ambapo karibu watu 600 walihudhuria hafla hizo.

Cai Qi, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Katibu wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC, akitembelea maonyesho yenye kaulimbiu ya "Kwa Ukombozi wa Taifa na Amani Duniani" mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 7, 2025. (Xinhua/Shen Hong)

Cai Qi, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Katibu wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC, akipeana mkono na wanajeshi wastaafu katika vita dhidi ya uvamizi wa Japan mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 7, 2025. (Xinhua/Shen Hong)

Picha iliyopigwa Julai 7, 2025 ikionyesha hafla ya kuadhimisha miaka 88 tangu kuanza kwa vita vya taifa zima dhidi ya uvamizi wa Japan, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 7, 2025. (Xinhua/Cai Yang)

Wanafunzi wakitoa heshima za maua kwa wale waliojitolea maisha yao katika kupigana dhidi ya uvamizi wa Japan kwenye Jumba la Makumbusho ya Vita vyaWatu wa China Dhidi ya Uvamizi wa Japan mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 7, 2025. (Xinhua/Chen Yehua)

Wanafunzi wakitoa heshima za maua kwa wale waliojitolea maisha yao katika kupigana dhidi ya uvamizi wa Japan kwenye Jumba la Makumbusho ya Vita vya Watu wa China Dhidi ya Uvamizi wa Japan mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 7, 2025. (Xinhua/Chen Yehua)

Wawakilishi wa wanajeshi wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China wakiwa wamesimama kwa ukimya kutoa heshima kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 88 tangu kuanza kwa vita vya taifa zima dhidi ya uvamizi wa Japan, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 7, 2025. (Xinhua/Cai Yang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha