

Lugha Nyingine
Rwanda yaandaa maadhimisho ya kikanda ya Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani
Maadhimisho ya Miaka Minne ya Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani yameanza Jumapili mjini Kigali, nchini Rwanda, yakiangazia jukumu la Kiswahili kama chachu ya mafungamano ya kikanda, elimu jumuishi na maendeleo endelevu.
Yakiandaliwa kwa pamoja na Rwanda na Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki, maadhimisho hayo ambayo yamefanyika kwa siku mbili yamepewa kaulimbiu ya “Kiswahili, Elimu Jumuishi na Maendeleo Endelevu”, yakihusisha uchunguzi wa sera zinazofaa, mbinu bora na ushirikishwaji wa wadau.
Hafla hiyo iliwaleta pamoja washiriki zaidi ya 300, wakiwemo maafisa waandamizi wa serikali, wajumbe kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wasomi, wataalamu wa Kiswahili na wanafunzi wa vyuo vikuu.
Akihutubia hafla hiyo Naibu Katibu Mkuu wa EAC Andrea Aguer Ariik Malueth amesema Kiswahili, mbali ya kuwa lugha, ni chombo cha usawa, ufikiaji na uwezeshaji.
Naye Waziri wa Nchi wa Rwanda anayeshughulikia Ushirikiano wa Kikanda James Kabarebe amesisitiza umuhimu wa Kiswahili katika kuendeleza umoja na maendeleo hasa ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma