Maandamano mapya nchini Kenya yasababisha vifo vya watu karibu 10 na wengine 28 kujeruhiwa

(CRI Online) Julai 08, 2025

Kamisheni ya Taifa juu ya Haki za Binadamu ya Kenya (KNCHR) imethibitisha kuwa watu takriban 10 wameuawa na wengine 29 kujeruhiwa jana Jumatatu wakati maafisa wa usalama walipokuwa wakipambana na waandamanaji katika duru mpya ya vurugu nchini kote.

KNCHR imeongeza kuwa maduka katika miji mikubwa yamefungwa kutokana na hofu ya uporaji na uharibifu na kwamba visa vya uporaji vimetokea katika kaunti sita na baadhi ya ofisi za serikali zimechomwa moto na watu wanaoshukiwa kuwa wahalifu katikati mwa Kenya.

Kamisheni hiyo imetoa taarifa ikisema kuwa polisi wameendelea kupuuzilia mbali amri ya Mahakama Kuu inayoamuru kwamba maafisa wote wanaosimamia maandamano wawe wamevalia sare rasmi na waendelee kutambulika wakati wote.

Katika taarifa yake, kamisheni hiyo imesema kuwa mamia ya watu wamekwama katika usafiri wa umma uliovurugika, ukiwemo wa ndege na reli, huku ikiongeza kuwa ilipokea simu za dharura kutoka kwa wagonjwa ambao hawakuweza kufikia vituo vya afya kutokana na kufungwa kwa barabara.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha