Moto kwenye kituo cha data cha Cairo wajeruhi 14, wasababisha kukatika kwa intaneti na mawasiliano ya simu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 08, 2025

Askari wa Zimamoto wakikabiliana na moto kwenye jengo la mawasiliano ya simu mjini Cairo, Misri, Julai 7, 2025 (Picha na Ismael Gomaa/Xinhua)

CAIRO - Moto umezuka jana Jumatatu ndani ya jengo la mawasiliano ya simu katika mji mkuu wa Misri, Cairo, ukijeruhi watu 14, na kusababisha huduma za mawasiliano ya simu na intaneti kukatika katika baadhi ya sehemu mjini humo ambapo majeruhi wamehamishiwa hospitali iliyo karibu kwa matibabu, Wizara ya Afya ya Misri imesema katika taarifa.

Shirika rasmi la habari la Misri, MENA limeripoti kuwa askari wa zimamoto walikuwa wamefanikiwa kuudhibiti moto huo katika jengo la Soko Kuu la Ramses, likiongeza kuwa shughuli za kuupoza zilikuwa zikiendelea muda huo ili kuhakikisha moto huo hauji kulipuka tena.

Chanzo cha kiusalama kimeliambia MENA kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa moto huo huenda umesababishwa na saketi fupi ya umeme, kikibainisha kuwa wataalam wa maabara ya uhalifu watakusanya ushahidi kutoka eneo la tukio ili kubaini sababu hasa.

Wakati huo huo, Mamlaka ya Taifa ya Kudhibiti Mawasiliano ya Misri imesema kuwa kazi inaendelea kutathmini kiwango cha uharibifu na kurejesha huduma hatua kwa hatua. 

Moshi ukifuka kupaa angani kutoka kwenye jengo la mawasiliano ya simu linaloungua mjini Cairo, Misri, Julai 7, 2025 (Picha na Ismael Gomaa/Xinhua)

Moshi ukifuka kupaa angani kutoka kwenye jengo la mawasiliano ya simu linaloungua mjini Cairo, Misri, Julai 7, 2025 (Picha na Ismael Gomaa/Xinhua)

Askari wa Zimamoto wakikabiliana na moto kwenye jengo la mawasiliano ya simu mjini Cairo, Misri, Julai 7, 2025 (Picha na Ismael Gomaa/Xinhua)

Askari wa Zimamoto wakikabiliana na moto kwenye jengo la mawasiliano ya simu mjini Cairo, Misri, Julai 7, 2025 (Picha na Ismael Gomaa/Xinhua)

Askari wa Zimamoto wakikabiliana na moto kwenye jengo la mawasiliano ya simu mjini Cairo, Misri, Julai 7, 2025 (Picha na Ismael Gomaa/Xinhua)

Askari wa Zimamoto wakikabiliana na moto kwenye jengo la mawasiliano ya simu mjini Cairo, Misri, Julai 7, 2025 (Picha na Ismael Gomaa/Xinhua)

Moshi ukifuka kupaa angani kutoka kwenye jengo la mawasiliano ya simu linaloungua mjini Cairo, Misri, Julai 7, 2025 (Picha na Ismael Gomaa/Xinhua)

Moshi ukifuka kupaa angani kutoka kwenye jengo la mawasiliano ya simu linaloungua mjini Cairo, Misri, Julai 7, 2025 (Picha na Ismael Gomaa/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha