Waziri Mkuu wa China asema uchumi wa China una uwezo wa kuhimili mishtuko yoyote ya nje

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 09, 2025

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria kongamano la kampuni za China zinazofanya shughuli zao nchini Brazil mjini Rio de Janeiro, Brazili, Julai 8, 2025. (Xinhua/Wang Ye)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria kongamano la kampuni za China zinazofanya shughuli zao nchini Brazil mjini Rio de Janeiro, Brazili, Julai 8, 2025. (Xinhua/Wang Ye)

RIO DE JANEIRO - Waziri Mkuu wa China Li Qiang jana Jumanne mjini Rio De Janeiro alipokutana na wawakilishi wa kampuni za China zinazofanya shughuli zao nchini Brazili amesema kuwa uchumi wa China una uwezo mkubwa wa kuhimili mishtuko yoyote ya nje na kufikia ukuaji thabiti wa muda mrefu.

Li amesema kuwa tangu mwanzo wa mwaka huu, uchumi wa China umesimama chini ya shinikizo na kudumisha mwelekeo wa maendeleo mazuri.

Washiriki wa mkutano huo ni pamoja na wakuu wa matawi wa Benki ya China, Kampuni ya magari ya Great Wall, Shirika la Gridi ya Taifa la China, kampuni ya sayansi na teknolojia ya Goldwind, kampuni ya chakula ya China, COFCO, Kampuni ya Vifaa vya Umeme vya Matumizi ya Nyumbani ya Gree, Kampuni ya teknolojia ya Dahua na Kundi la ZTT.

Baada ya kusikiliza maelezo ya washiriki, Li amesema kuwa katika miaka ya hivi karibuni, kampuni za China zimekuwa zikiongeza kasi ya kupanua shughuli zao katika nchi za nje na kuboresha uwezo wao wa shughuli za kimataifa, na kuchukua nafasi muhimu katika kukuza uchumi wa ndani.

Li amesema katika nusu ya kwanza ya mwaka huu uchumi wa China umeongezeka kwa uhimilivu mkubwa huku ukiwa na mahitaji makubwa ya ndani na maeneo muhimu kichocheo na yanayokua kwa kasi katika uvumbuzi.

Akisema kuwa uchumi wa China daima utatoa uungaji mkono mkubwa kwa kampuni za China zinazofanya shughuli zao ng'ambo, Waziri Mkuu huyo amesema serikali itatoa huduma bora na dhamana kwa kampuni, kuimarisha ujenzi wa mifumo na majukwaa mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, na kuboresha mfumo jumuishi wa huduma nje ya nchi.

“Hali ya sasa ya uchumi na biashara ya kimataifa inabadilika sana huku kukiwa na kuongezeka kwa hatua za upande mmoja na za kujilinda kibiashara, na kuongezeka kwa vizuizi vya biashara na uwekezaji,” Li amesema.

Amesema anatumai kampuni za China zinaweza kubadilika ili kuendana na mwelekeo huo, na kuchukua hatua za haraka na kwamba zinapaswa kujenga chapa zenye nguvu, kuimarisha mipango, na kuongeza uwezo wa kushindana kimataifa wa "Made in China" na "Created in China".

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha