China yapenda kushirikiana na Umoja wa Mataifa kuhimiza utaratibu wa kimataifa wenye haki na usawa zaidi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 09, 2025

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres mjini Rio de Janeiro, Brazili, Julai 8, 2025. (Xinhua/Yao Dawei)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres mjini Rio de Janeiro, Brazili, Julai 8, 2025. (Xinhua/Yao Dawei)

RIO DE JANEIRO - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema China inapenda kuzidisha uratibu na ushirikiano kati yake na Umoja wa Mataifa ili kwa pamoja kuhimiza utaratibu wa kimataifa uwe na haki na usawa zaidi, wakati alipokutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres pembezoni mwa Mkutano wa 17 wa Kilele wa BRICS jana Jumanne mjini Rio De Janeiro, Brazil.

"Katika kipindi cha miaka 80 iliyopita tangu kuanzishwa kwake, Umoja wa Mataifa umetoa mchango mkubwaa katika kulinda amani na utulivu duniani huku ukihimiza maendeleo ya pamoja," Li amesema.

Huku akionya kwamba dunia inakabiliwa na kuongezeka kwa mambo yasiyo ya utulivu na hali ya kutokuwa na uhakika, Li amesema kuwa Umoja wa Mataifa unahitaji kuchukua jukumu bora zaidi.

Amesisitiza kuwa, maono ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu na mapendekezo makuu matatu ya dunia, yiliyopendekezwa na Rais Xi Jinping wa China, vinaendana sana na madhumuni na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa, kwani vinajumuisha dhamira thabiti na mtazamo wa kivitendo wa China kuunga mkono mfumo wa pande nyingi na kazi ya Umoja wa Mataifa.

“Kadri hali ya kimataifa inavyozidi kuwa ngumu, ndivyo inavyohitajika zaidi kushikilia mamlaka ya Umoja wa Mataifa,” amesema Li, akieleza kwamba China inaunga mkono kithabiti jukumu kuu la Umoja wa Mataifa katika usimamizi wa dunia na inapenda kushirikiana na pande zote kutekeleza ushirikiano wa kweli wa pande nyingi na kuhimiza kazi ya Umoja wa Mataifa kupata maendeleo makubwa zaidi.

Kwa upande wake, Guterres ameelezea shukrani zake kwa China kushikilia ushirikiano wa pande nyingi kwa muda mrefu, vilevile uungaji mkono wake thabiti kwa kazi ya Umoja wa Mataifa.

Bw. Guterrez amesema kuwa mapendekezo matatu ya dunia yaliyotolewa na Rais Xi yanaendana na malengo ya Umoja wa Mataifa na kwamba kutokana na hali ya sasa ya kimataifa, Umoja wa Mataifa unatarajia kuchukua maadhimisho ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwake kama fursa ya kuimarisha ushirikiano na China, kulinda mamlaka ya Katiba ya Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa, kuunga mkono ushirikiano wa pande nyingi, kupinga maamuzi ya upande mmoja, kwa pamoja kushughulikia mabadiliko ya Tabianchi na changamoto nyinginezo duniani.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres mjini Rio de Janeiro, Brazili, Julai 8, 2025. (Xinhua/Yao Dawei)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres mjini Rio de Janeiro, Brazili, Julai 8, 2025. (Xinhua/Yao Dawei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha