EAC na IGAD zashirikiana katika kuhimiza malipo ya kidigitali ya kuvuka mpaka

(CRI Online) Julai 09, 2025

Makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yametoa taarifa jana Jumanne ikisema kuwa jumuiya hiyo na Mamlaka ya Kiserikali kwa Maendeleo ya Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) zimepiga hatua muhimu katika kuunganisha masoko ya kidigitali ya kanda hiyo.

Taarifa hiyo inafuatia kongamano la ngazi ya juu lililofanyika chini ya Mradi wa Mafungamano ya Kidigitali ya Afrika Mashariki (EARDIP), ambao ni mpango muhimu unaotekelezwa kwa pamoja na IGAD na EAC zikiungwa mkono na Benki ya Dunia.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mradi wa EARDIP unalenga kuharakisha mafungamano ya kidigitali ya kanda hiyo kupitia kupanua miundombinu ya intaneti ya kasi ya Broadband na kuimarisha mazingira ya kiusimamizi kwa huduma za kidigitali za kuvuka mpaka, hasa malipo ya kidigitali ambayo ni kichocheo muhimu cha biashara, utumaji fedha kutoka nje, na ujumuishaji wa kifedha.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha