

Lugha Nyingine
Rais Xi ahutubia Mkutano wa Kazi ya Miji ya Kamati Kuu ya Chama na kubainisha kazi muhimu ya maendeleo ya miji
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu kwenye Mkutano wa Kazi ya Miji ya Kamati Kuu ya Chama mjini Beijing. (Xinhua/Xie Huanchi)
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba muhimu kwenye Mkutano wa Kazi ya Miji ya Kamati Kuu ya Chama uliofanyika Beijing kuanzia Jumatatu hadi Jumanne, na wajumbe wa kudumiu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang na Li Xi pia wamehudhuria mkutano huo, ambapo Xi ametoa matakwa ya jumla, kanuni muhimu na majukumu ya kipaumbele kuhusu kazi ya miji.
Mkutano huo umesema kuwa, tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama cha CPC mwaka 2012, Kamati Kuu ya Chama imekuwa ikishikilia kuendeleza miji ya umma, kuendeleza miji kwa ajili ya umma, na kuendeleza miji inayojengwa na umma, na ujenzi wa miji umepata mafanikio ya kihistoria.
"Ukuaji wa miji wa China unabadilika kutoka ukuaji wa kasi hadi maendeleo tulivu, na maendeleo ya miji yanabadilika kutoka hatua ya upanuzi wa kiwango kikubwa hadi yale yanayotilia maanani zaidi kuongeza ubora na ufanisi wa maeneo ya mijini yaliyopo," mkutano huo umesema.
Mkutano huo umetoa matakwa ya jumla kuhusu kazi ya miji kwa hivi sasa na kwa siku za baadaye, yakiwemo kujenga miji ya kisasa ya kivumbuzi, inayofaa kuishi, inayopendeza, inayoweza kuvumilia hali yoyote, inayofuata ustaarabu, na uendeshaji wa teknolojia ya hali ya juu, ili kufuata njia mpya ya mambo ya kisasa ya miji yenye umaalum wa China.
Msisitizo mkubwa lazima uwekwe katika kutoa kipaumbele cha juu kwa watu, kujenga sifa za kipekee, kuongeza uwezo wa usimamizi, na kuimarisha uratibu, mkutano huo umesema.
Vipaumbele muhimu kwa maendeleo ya miji vinahusisha kuboresha mfumo wa kisasa wa miji, kujenga miji yenye hali moto moto inayowezeshwa na uvumbuzi, na kujenga mazingira ya kuishi yaliyo tulivu na urahisi kwa maisha, vilevile kuhimiza maeneo ya mijini yaliyo ya kijani, kaboni chache na ya kupendeza, mkutano huo umeeleza.
Mkutano huo umesisitiza kuwa kujenga miji ya kisasa kwa ajili ya watu kunahitaji kuimarisha uongozi mzima wa Chama cha CPC juu ya kazi husika.
Li Qiang alitoa hotuba ya kuhitimisha mkutano huo.
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu kwenye Mkutano wa Kazi ya Miji ya Kamati Kuu ya Chama mjini Beijing . (Xinhua/Xie Huanchi)
Li Qiang, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Kisiasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akitoa hotuba kwenye Mkutano wa Kazi ya Miji ya Kamati Kuu ya Chama mjini Beijing . (Xinhua/Yue Yuewei)
Wilaya ya Xuan’en yahimiza utalii wa usiku kando ya Mto Gongshui Katikati mwa China
Eneo la mtaa mkongwe lawa na ustawi kwa uvumbuzi wa kitamaduni na utalii mkoani Jiangxi, China
Mji wa Tianjin, China waharakisha ufungamanishaji wa uchumi wa kidijitali na uchumi halisi
Ardhioevu yalinda spishi za ndege kutoka kwenye uwanda hadi mijini
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma