Rais Xi Jinping akutana na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese mjini Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 16, 2025

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 15, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 15, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amekutana na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese mjini Beijing jana Jumanne, ambapo kwa mara nyingine tena amempongeza Albanese kwa kuchaguliwa tena, akisema kwamba kwa juhudi za pamoja za pande zote mbili, uhusiano kati ya China na Australia umeibuka kutoka hali mbaya na kupata mabadiliko katika miaka ya hivi karibuni, ukileta manufaa halisi kwa watu wa nchi zote mbili.

"Jambo muhimu zaidi ambalo tulichopata ni kwamba kutendeana kwa usawa, kutafuta maelewano wakati kuondoa tofauti, na kushiriki katika ushirikiano wa kunufaishana kunatumikia maslahi ya kimsingi ya China na Australia na watu wao," Rais Xi amesema.

Akisema kuwa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Australia umeingia katika muongo wake wa pili, Rais Xi amesema China inapenda kushirikiana na Australia kuhimiza uhusiano kati yao kuendelezwa vizuri ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wao.

Akiongeza kuwa China na Australia zinapaswa kuendelea kuongeza hali ya kuaminiana kimkakati, Rais Xi amesisitiza dhamira isiyoyumbayumba ya China kwa maendeleo ya amani, kufanya juhudi kwa ajili ya kupata maendeleo kwa pamoja, na kuhimiza ushirikiano wa Asia na Pasifiki.

Rais Xi pia ametoa wito kwa nchi hizo mbili kuzidisha na kupanua ushirikiano wao wa kunufaishana, akisema kuwa China imekuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Australia kwa miaka 16 mfululizo na biashara yake na China imeleta manufaa halisi kwa Australia.

Akisisitiza umuhimu wa kukuza uhusiano kati ya watu na watu, Rais Xi amesema China inakaribisha Waaustralia wa sekta mbalimbali kutembelea nchi hiyo na inapenda kualika vijana zaidi wa Australia kuja kushiriki programu za mawasiliano.

Ametoa wito kwa pande zote mbili kushughulikia kwa pamoja hatari na changamoto, kushikilia haki na usawa wa kimataifa, kulinda mfumo wa pande nyingi na biashara huria, na kutetea mfumo wa kimataifa huku Umoja wa Mataifa ukiwa ndiyo msingi wake na utaratibu wa kimataifa unaozingatia sheria za kimataifa.

Kwa upande wake Albanese amesema kuwa Australia inathamini uhusiano wake na China na inatarajia kushirikiana na China ili kutendeana kwa usawa, kutafuta maelewano wakati kuondoa tofauti, na kushiriki katika ushirikiano wa kunufaishana ili kuhimiza uhusiano wa pande mbili kupata maendeleo mapya.

Akisema kuwa Australia inashikilia sera ya kuwepo kwa China moja na haiungi mkono "Taiwan ijitenge," amesema Australia inapenda kudumisha mazungumzo na mawasiliano na China katika ngazi zote ili kuongeza hali ya kuaminiana. 

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 15, 2025. (Xinhua/Yin Bogu)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 15, 2025. (Xinhua/Yin Bogu)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha