Rais Xi atuma salamu za rambirambi kwa kifo cha Rais wa zamani wa Nigeria Buhari

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 17, 2025

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping jana Jumatano ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Nigeria Bola Tinubu kutokana na kifo cha Rais wa zamani wa Nigeria Muhammadu Buhari, ambapo akiwa kwa niaba ya serikali ya China na watu wa China, Rais Xi ameelezea huzuni kubwa na kutoa pole ya dhati kwa familia ya Buhari, serikali na watu wa Nigeria.

Rais Xi amesema kuwa Buhari alikuwa kiongozi muhimu wa Nigeria, ambaye alijikita katika kutafuta njia ya maendeleo inayolingana na hali ya nchi yake, na kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya mshikamano na maendeleo ya makabila ya nchi yake, na anaheshimiwa sana katika jumuiya ya kimataifa.

Rais Xi amesema, Buhari alilinda kithabiti urafiki na China, na alifanya juhudi za kuhimiza urafiki kati ya Nigeria na China na ushirikiano kati ya China na Afrika. Kifo chake ni hasara kubwa kwa watu wa Nigeria, na watu wa China wamepoteza rafiki mpendwa.

"China inatilia maanani sana kuendeleza uhusiano wake na Nigeria na inapenda kushirikiana na na upande wa Nigeria ili kuhimiza siku hadi siku uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote," Rais Xi amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha