

Lugha Nyingine
China yaripoti kuongezeka kwa watalii wa kigeni kutokana na sera iliyopanuliwa ya bila visa
Watalii kutoka Australia watembelea Hekalu ya Tiantan mjini Beijing, mji mkuu wa China, Mei 1, 2025. (Xinhua/Ju Huanzong)
BEIJING - Idadi inayoongezeka ya watalii wa kigeni wamekuja China katika nusu ya kwanza ya mwaka 2025, ikisababishwa kwa sehemu na utaratibu unaolegezwa wa viza -- hasa upanuzi wa programu za kusafiri bila kuomba visa za nchi hiyo.
Wageni walifanya safari jumla ya milioni 38.05 kwenda au kutoka China katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu, ambayo ilikuwa ongezeko la asilimia 30.2 kuliko mwaka jana wakati kama huo, Mamlaka ya Taifa ya Uhamiaji ya China (NIA) imesema jana Jumatano.
"Kati ya safari hizi, milioni 13.64 zilikuwa za uingiaji China bila visa, ongezeko la asilimia 53.9 kuliko kipindi kama hicho mwaka jana," NIA imesema.
Lyu Ning, msemaji wa NIA, amesema ongezeko hilo linatokana na juhudi za China za kurahisisha utaratibu wa visa katika miaka ya hivi karibuni, akisema kuwa hatua zake zimevutia wageni wa kimataifa wanaokuja nchini kwa safari za utalii au biashara.
Hivi karibuni, China ilitia saini makubaliano ya kusameheana visa na Uzbekistan, Malaysia na Azerbaijan, na imetoa sera ya msamaha huo kwa upande mmoja kwa nchi tisa zaidi, zikiwemo Brazil, Argentina na Chile.
Makubaliano kati ya China na Azerbaijan, ambayo yanahusu wamiliki wa pasipoti za kawaida kutoka nchi hizo mbili, yameanza kutekelezwa jana Jumatano ambapo Raia wa China au Azerbaijan ambao wana pasipoti halali ya kawaida wataweza kuingia, kutoka au kuunganisha ndege kwenda nchi nyingine nchini China bila visa.
Chini ya mpango huo, kuingia na kuwepo kwa mara moja katika nchi husika hakupaswi kuzidi siku 30, na kuwepo nchini kwa jumla ya siku zisizozidi 90 kunaruhusiwa ndani ya kipindi chochote cha siku 180.
Aidha, raia wa nchi 55, zikiwemo Marekani na Canada, wanaweza kutembelea China bila visa kwa hadi siku 10 kwa kuunganisha ndege kwenda nchi nyingine, kabla ya kusafiri hadi nchi au eneo la tatu.
Mabadiliko haya makubwa ya sera yamewezesha watu kusafiri China, ikisababisha kuongezeka kwa maudhui ya mtandaoni na mambo yanayovutia kuhusu "Kusafiri China," hasa kwenye majukwaa ya mtandaoni kama vile YouTube.
Picha hii ikionyesha duka lisilotoza kodi katika Mji wa Chongqing, kusini-magharibi mwa China, Mei 2, 2025. (Xinhua/Huang Wei)
Wilaya ya Xuan’en yahimiza utalii wa usiku kando ya Mto Gongshui Katikati mwa China
Eneo la mtaa mkongwe lawa na ustawi kwa uvumbuzi wa kitamaduni na utalii mkoani Jiangxi, China
Mji wa Tianjin, China waharakisha ufungamanishaji wa uchumi wa kidijitali na uchumi halisi
Ardhioevu yalinda spishi za ndege kutoka kwenye uwanda hadi mijini
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma