

Lugha Nyingine
Uwanja wa ndege wa Xinjiang, China warekodi ongezeko kubwa la safari za abiria za kuvuka mpaka huku kukiwa na msukumo wa kufungua mlango
![]() |
Abiria wakionekana kwenye ukumbi wa kuondokea wa kituo kipya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Tianshan mjini Urumqi, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China, Aprili 17, 2025. (Xinhua/Wang Fei) |
URUMQI - Jumla ya abiria 500,000 za kuingia au kutoka China zimerekodiwa mwaka 2025 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Tianshan mjini Urumqi, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China -- idadi kubwa zaidi katika kipindi cha Januari-Julai katika muongo mmoja.
Hadi kufikia Jumatatu, abiria wa kigeni walikuwa wamefanya safari zaidi ya 146,000 kuingia China kupitia uwanja huo wa ndege mwaka huu, ambayo ni ongezeko la asilimia 30 kuliko mwaka jana wakati kama huo, kwa mujibu wa takwimu za mamlaka za uhamiaji kwenye uwanja huo. Miongoni mwa safari hizo, 39,000 zilikuwa za uingiaji bila visa.
Asilimia takriban 40 ya abiria hao wa kigeni walikuwa wakisafiri kwa ajili ya utalii, mamlaka hizo za uhamiaji zimesema, zikiongeza kuwa biashara na kutembelea jamaa au marafiki ni sababu za pili na tatu za mara kwa mara za kuingia kuvuka mpaka miongoni mwa abiria hao wa kigeni.
Uwezo wa kupokea abiria na kushughulikia mizigo katika uwanja huo wa ndege uliongezeka kwa kiasi kikubwa wakati kituo kipya cha uwanja wa ndege huo kilipoanza kufanya kazi miezi mitatu iliyopita ambapo kituo hicho kipya ni sehemu muhimu ya mradi wa upanuzi wa uwanja huo ulioanza mwaka 2019.
Kwa upanuzi huo, uwanja huo wa ndege sasa una njia tatu za ndege kuruka na kutua -- ongezeko kubwa kutoka njia moja ya awali -- na unaweza kupokea abiria hadi milioni 48 na kushughulikia tani 550,000 za mizigo kwa mwaka. Sasa una uwezo wa kuunga mkono kupaa na kutua kwa ndege karibu 367,000 kwa mwaka.
"Kama kituo cha usafiri wa anga kwa China kufungua mlango kuelekea magharibi, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Tianshan mjini Urumqi unapiga hatua katika pande mbalimbali, ukiunga mkono ufunguaji mlango wa kiwango cha juu wa eneo la kaskazini-magharibi mwa nchi," amesema He Mingxing, msomi katika Chuo Kikuu cha Xinjiang.
Kituo hicho kipya ni kiwakilishi cha maendeleo ya haraka ya miundombinu ya usafiri wa anga katika mkoa huo wa Xinjiang.
Na kutokana na Uwanja wa Ndege wa Barkol Dahe mkoani humo kuanza kazi rasmi Jumanne wiki hii, jumla ya idadi ya viwanja vya ndege vya kiraia vya Xinjiang imepanda hadi 28 – idadi kubwa zaidi kati ya maeneo yote ya ngazi ya mkoa nchini China.
Wilaya ya Xuan’en yahimiza utalii wa usiku kando ya Mto Gongshui Katikati mwa China
Eneo la mtaa mkongwe lawa na ustawi kwa uvumbuzi wa kitamaduni na utalii mkoani Jiangxi, China
Mji wa Tianjin, China waharakisha ufungamanishaji wa uchumi wa kidijitali na uchumi halisi
Ardhioevu yalinda spishi za ndege kutoka kwenye uwanda hadi mijini
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma