Mashindano Makubwa ya AI Kuwezesha Sekta Mbalimbali yazinduliwa Nanning, Guangxi, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 19, 2025

Leo Jumamosi, Julai 19, Mashindano Makubwa ya AI Kuwezesha Sekta Mbalimbali yamezinduliwa Nanning, Guangxi, China.

Mashindano hayo, yenye kaulimbiu ya "AI Guangxi, AI China, AI ASEAN", yatadumu kuanzia Julai hadi Novemba, yakivutia kampuni ongozi za ndani na nje ya China, timu za utafiti wa kisayansi, wanafunzi wa vyuo vikuu na wabunifu binafsi wa programu za kompyuta kushiriki. Washiriki wamechunguza kikamilifu muktadha wa matumizi ya AI, kusisitiza kukuza kampuni zinazoibuka za AI kwa soko la ASEAN, kuhimiza mafungamano ya kina ya teknolojia ya AI na uchumi halisi, kuhimiza mageuzi ya AI kuwa nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora na kuwezesha sekta mbalimbali.

Picha ikionyesha hafla ya uzinduzi. (Picha na Yan Lizheng/People's Daily Online)

Picha ikionyesha hafla ya uzinduzi. (Picha na Yan Lizheng/People's Daily Online)

Mashindano hayo yameweka vipengele vitatu vikuu: Mashindano ya Uvumbuzi wa Matumizi ya AI, Mashindano ya Matumizi ya AI katika sekta maalumu, na Mashindano ya AI kwa watu wa kawaida.

Pia mashindano yameweka vipengele vidogo mbalimbali vianvyohusu sekta 17 muhimu, kama vile AI+Magari, Vipaji vya Ng'ambo, Biashara ya Mtandaoni ya Kuvuka Mipaka, Utamaduni na Utalii wa Teknolojia za Kisasa, na Kilimo cha Teknolojia za kisasa, ili kuchunguza utatuzi wa kivumbuzi ambao unaweza kutekelezwa haraka na kutumika kwa eneo pana, na kuyafanya maendeleo ya AI yaipe kipaumbele maanani watu na kunufaisha watu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha