

Lugha Nyingine
Rais Xi na mwenzake wa Mauritania Ghazouani wapongezana kwa maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Mauritania Mohamed Ould Cheikh Ghazouani walitumiana salamu za pongezi juzi Jumamosi kwa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, ambapo kwenye pongezi lake Rais Xi amesema, katika miaka 60 iliyopita, bila kujali mazingira ya kimataifa yalivyobadilika kwa namna gani, pande hizo mbili zimekuwa zikiheshimiana na kutendeana kwa usawa, zikiweka mfano wa kuungana mkono na kufanya ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi zinazoendelea.
Amesema kuwa katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya China na Mauritania umekuwa ukiendelea vizuri na kwa utulivu, ambapo hali ya kuaminiana kisiasa imeimarishwa siku hadi siku, na mafanikio makubwa yamepatikana katika mawasiliano na ushirikiano katika sekta mbalimbali.
Rais Xi amekumbuka kuwa alikutana na Rais Ghazouani mwaka jana wakati wa Mkutano wa Kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), ambapo walifikia makubaliano muhimu na kutangaza kwa pamoja kuinua uhusiano kati ya China na Mauritania hadi kuwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati, ikimaanisha ukurasa mpya wa uhusiano wa pande mbili.
Rais Xi amesema ametilia maanani zaidi kuendeleza uhusiano kati ya China na Mauritania na anapenda kushirikiana na Ghazouani kuchukua maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kuwa mwanzo mpya wa kuenzi urafiki wa jadi, kuzidisha hali ya kuaminiana na ushirikiano, na kwa pamoja kufungua mustakabali mpya kwa maendeleo ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Mauritania, ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili.
Kwa upande wake, Rais Ghazouani amesema katika miaka 60 iliyopita, nchi yake na China zimeendeleza ushirikiano wa karibu katika ngazi zote, kuungana mkono juu ya masuala ya kimataifa, na zimekuwa na urafiki mkubwa.
Ghazuoani amesema, wakati wa Mkutano wa kilele wa FOCAC wa Beijing mwezi Septemba mwaka jana, yeye na Rais Xi kwa pamoja waliinua uhusiano wa pande mbili wa mfano wa kuigwa hadi kuwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati, hatua hiyo ni ishara ya kuendelezwa kwa kina kwa uhusiano wa pande mbili, ambayo itanufaisha watu rafiki wa nchi hizo mbili, na kusaidia kuhimiza usalama, ustawi na manufaa kwa watu duniani.
Siku hiyo hiyo, Waziri Mkuu wa China Li Qiang na mwenzake wa Mauritania, Mokhtar Ould Diay pia walitumiana salamu za pongezi.
Wilaya ya Xuan’en yahimiza utalii wa usiku kando ya Mto Gongshui Katikati mwa China
Eneo la mtaa mkongwe lawa na ustawi kwa uvumbuzi wa kitamaduni na utalii mkoani Jiangxi, China
Mji wa Tianjin, China waharakisha ufungamanishaji wa uchumi wa kidijitali na uchumi halisi
Ardhioevu yalinda spishi za ndege kutoka kwenye uwanda hadi mijini
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma