

Lugha Nyingine
China na Mauritania zaadhimisha miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia mjini Nouakchott
Mohamed Salem Ould Merzoug, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritania, anayeshughulikia Mambo ya Nje, Ushirikiano na Wamauritania walioko nje ya nchi, akizungumza kwenye tafrija ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Mauritania mjini Nouakchott, Mauritania, Julai 18, 2025. (Xinhua/Han Xu)
NOUAKCHOTT - Ubalozi wa China nchini Mauritania uliandaa tafrija siku ya Ijumaa kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Nouakchott, kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Mauritania.
Tafrija hiyo iliwaleta pamoja wageni wapatao 300, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritania, anayeshughulikia Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika na Wamauritania walioko nje ya nchi Mohamed Mauritania, Balozi wa China nchini Mauritania Tang Zhongdong, wawakilishi kutoka sekta mbalimbali, wanadiplomasia wa kigeni, vilevile wanachama wa jumuiya ya Wachina nchini humo.
Akizungumza kwa niaba ya Rais wa Mauritania Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani, Merzoug amesema kuwa katika miongo sita iliyopita, uhusiano kati ya Mauritania na China umeendelea kwa kasi tulivu juu ya msingi wa kuheshimiana, kutoingiliana mambo ya ndani, na ushirikiano wa kunufaishana, na kuwa mfano wa kuigwa kwa ushirikiano wa Kusini na Kusini.
Amesisitiza tena uungaji mkono thabiti wa Mauritania kwa kanuni ya kuwepo kwa China moja na kuelezea shukrani kwa mchango wa China katika sekta mbalimbali nchini Mauritania.
“Mauritania imedhamiria kuimarisha uratibu na China katika masuala ya kimataifa, kuzidisha ushirikiano wa kivitendo, na kuhimiza zaidi ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili” ameongeza.
Kwa upande wake Balozi wa China alifanya majumuisho ya upigaji hatua kwa uhusiano wa pande mbili katika miaka hiyo 60 iliyopita, akisisitiza kuongezeka hali ya kuaminiana kisiasa, kupanua ushirikiano, na mawasiliano moto moto kati ya watu na watu.
"China inapenda kushirikiana na Mauritania kutekeleza maafikiano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili, na kuendelea kuungana mkono chini ya mifumokazi kama vile Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika na Baraza la Ushirikiano la China na Nchi za Kiarabu, ili kuleta manufaa halisi kwa nchi zote mbili," Tang amesema.
Tafrija hiyo imefanyika katika hali ya upendo na shwari. Wageni waalikwa pia walitembelea maonyesho ya picha ya "Lenzi ya Xinhua, Taswira za Karne", yaliyozinduliwa siku hiyo hiyo katika kituo hicho cha mikutano.
Yakiwa yameandaliwa kwa pamoja na Ubalozi wa China nchini Mauritania na Kituo cha Shirika la Habari la China, Xinhua barani Afrika, Maonyesho hayo yataendelea hadi Oktoba na yatakuwa yakifanyika katika maeneo kadhaa, ikiwemo Kituo cha Kimataifa cha Mikutano, Ubalozi wa China na Akademia ya Kidiplomasia ya Mauritania.
Balozi wa China nchini Mauritania Tang Zhongdong, akizungumza kwenye tafrija ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Mauritania mjini Nouakchott, Mauritania, Julai 18, 2025. (Xinhua/Han Xu)
Wilaya ya Xuan’en yahimiza utalii wa usiku kando ya Mto Gongshui Katikati mwa China
Eneo la mtaa mkongwe lawa na ustawi kwa uvumbuzi wa kitamaduni na utalii mkoani Jiangxi, China
Mji wa Tianjin, China waharakisha ufungamanishaji wa uchumi wa kidijitali na uchumi halisi
Ardhioevu yalinda spishi za ndege kutoka kwenye uwanda hadi mijini
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma