Watu takriban 19 wafariki dunia baada ajali ya kuanguka kwa ndege ya Jeshi la Bangladesh

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 22, 2025

Askari wa zimamoto wakifanya kazi kwenye eneo la ajali mjini Dhaka, Bangladesh, Julai 21, 2025. (Xinhua)

Askari wa zimamoto wakifanya kazi kwenye eneo la ajali mjini Dhaka, Bangladesh, Julai 21, 2025. (Xinhua)

DHAKA - Watu takriban 19, wengi wao wakiwa wanafunzi, wamefariki dunia baada ya ndege ya mafunzo ya Kikosi cha Anga cha Jeshi la Bangladesh kuanguka kwenye kampasi ya chuo mjini Dhaka, Bangladesh jana Jumatatu, ambapo taarifa ya serikali imesema kuwa watu zaidi ya 100 wamejeruhiwa katika ajali hiyo na wengi wao wako katika hali mbaya.

Idara ya Huduma za Uhusiano kwa Umma (ISPR) ya Jeshi la Bangladesh imesema ndege hiyo ya mafunzo ilianguka majira ya 7:30 mchana kwa saa za Bangladesh. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha