Maonesho ya Ngoma ya kijadi ya Dakpo Axie yafanyika kwenye eneo la vivutio vya utalii la Nagqu, Xizang, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 21, 2025
Maonesho ya Ngoma ya kijadi ya Dakpo Axie yafanyika kwenye eneo la vivutio vya utalii la Nagqu, Xizang, China
Wasanii wa kundi la michezo ya sanaa la Wilaya ya Biru wakicheza ngoma ya kijadi ya Dakpo Axie, ambayo ni mali ya urithi wa utamaduni usioshikika wa kitaifa wa China, kwenye eneo la vivutio vya utalii la Mlima Sapukonglagabo katika Wilaya ya Biru huko Nagqu, Mkoa unaojiendesha wa Xizang, kusini-magharibi mwa China, Julai 19, 2025.

Kundi la michezo ya sanaa la Wilaya ya Biru limekuwa likicheza ngoma ya kijadi ya Dakpo Axie, ambayo ni maonesho ya sita ya mali ya kitaifa ya urithi wa utamaduni usioshikika wa China yaliyochezwa na kundi hilo mwaka huu katika eneo la vivutio vya utalii la Mlima Sapukonglagabo.

Katika miaka ya hivi karibuni, Mji wa Nagqu umefanya juhudi kubwa za kuhimiza mafungamano kati ya urithi wa utamaduni usioshikika na utalii. Watalii sasa wamekuwa na fursa zaidi za kutazama maonyesho ya michezo ya sanaa inayohusu mali ya urithi wa utamaduni usioshikika kwenye maeneo ya vivutio vya utalii wakati wa likizo na msimu wa kilele cha utalii. (Xinhua/Jigme Dorje)(Xinhua/Jigme Dorje)

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha