

Lugha Nyingine
Makamanda wa vyuo vya kijeshi vya Afrika wakutana Rwanda kuimarisha ushirikiano
Mkutano wa wakufunzi wakuu kutoka vyuo vya ukamanda na unadhimu vya nchi 18 za Afrika umefunguliwa Jumatatu mjini Kigali, ukilenga kuimarisha ushirikiano kati ya vyuo hivyo na kuboresha ubora na umuhimu wa mafunzo na elimu inayotolewa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Rwanda, mkutano huo, utakaofanyika mpaka kesho Alhamisi, unatarajiwa kufikia uelewa wa pamoja kuhusu matishio yanayoibuka na uhalisia wa kioperesheni.
Akifungua mkutano huo, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Rwanda Mubarakh Muganga amesisitiza umuhimu wa kuwawezesha maofisa wa kijeshi kuwa na viwango vya juu vya kitaaluma na kitaalamu, pamoja na hitaji la kufanya operesheni za pamoja katika kanda tofauti.
Bw. Muganga amerejea tena ahadi ya Rwanda ya kushirikiana na nchi zote wanachama katika kuimarisha ushirikiano, kuwianisha mtaala wa mafunzo, na kuingiza uvumbuzi wa kidijitali kwenye mifumo ya mafunzo ya kijeshi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma