Maliasili nyingi za chumvi zaongeza mapato ya wanakijiji katika Wilaya ya Gegye, Xizang, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 22, 2025
Maliasili nyingi za chumvi zaongeza mapato ya wanakijiji katika Wilaya ya Gegye, Xizang, China
Picha hii iliyopigwa Julai 20, 2025 ikionyesha bidhaa za kiwanda cha kuchakata chumvi ghafi katika Wilaya ya Gegye ya Eneo la Ngari, Mkoa unaojiendesha wa Xizang, kusini-magharibi mwa China. (Xinhua/Tenzing Nima Qadhup)

Wilaya ya Gegye ya Eneo la Ngari katika Mkoa unaojiendesha wa Xizang, kusini-magharibi mwa China ni sehemu yenye maliasili nyingi za chumvi. Wilaya hiyo imeanzisha kiwanda cha kuchakata chumvi ghafi, na inaunda hatua kwa hatua mnyororo wa uzalishaji wa kiwanda hicho unaohusisha kazi za uvunaji, uhifadhi, uchakataji, ufungashaji na uuzaji chumvi, ili kuongeza mapato ya wanakijiji. Mwaka 2018, desturi ya wilaya hiyo ya kondoo kubeba chumvi iliwekwa kwenye orodha ya uwakilishi wa mali ya urithi wa utamaduni usioshikika ya Mkoa huo unaojiendesha wa Xizang.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha