

Lugha Nyingine
Namibia yapanga upanuzi mkubwa wa mashamba, na ongezeko la mauzo ya nje ya mazao ya kilimo ifikapo 2030
Namibia inapanga kupanua mashamba makubwa ya kilimo na kuongeza thamani ya mauzo ya nje ya mazao kilimo ya kimkakati, ili kuimarisha usalama wa chakula, kukuza sekta ya kilimo, na kuongeza mapato ya vijijini ifikapo 2030, ikiwa ni sehemu ya mpango wake mpya wa maendeleo wa kitaifa.
Mpango huo unaojulikana kwa jina la Mpango wa Sita wa Maendeleo ya Kitaifa (NDP6), ulizinduliwa Jumatatu na Rais Netumbo Nandi-Ndaitwah ili kuongoza sera za kiuchumi na kijamii kutoka 2025 hadi 2030.
Kwa mujibu wa mpango huo, serikali itaongeza eneo la uzalishaji mkubwa wa mazao kutoka hekta 11,200 za mwaka 2024 hadi hekta 130,000 ifikapo mwaka 2030, ikiwa ni sehemu muhimu ya jitihada kubwa za kufanya kilimo kuwa cha kisasa na kuongeza uwezo wa nchi hiyo kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Mpango huo pia unaweka lengo la kuongeza thamani ya mauzo ya mazao ya kimkakati kutoka dola bilioni 1.9 za Namibia hadi dola bilioni 2.8 za Namibia katika kipindi hicho.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma