

Lugha Nyingine
Watia nia ya kugombea urais kurudisha fomu za uteuzi kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Malawi
Wagombea 20 ambao wamechukua fomu kutoka Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC) za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi katika kinyang'anyiro cha urais wa Septemba 16 wanatarajiwa kurudisha fomu zao kwa tume ya uchaguzi kuanzia Julai 24 hadi 30.
Wagombea hao ni pamoja na Rais anayemaliza muda wake Bw. Lazarus Chakwera wa chama tawala cha Malawi Congress Party, rais wa zamani Bw. Peter Mutharika wa Chama cha Democratic Progressive Party, rais wa zamani Bibi Joyce Banda na chama cha People's Party, na gavana wa zamani wa benki kuu ya Malawi Bw. Dalitso Kabambe wa chama cha United Transformation Movement.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa Jumatatu na tume ya uchaguzi, Bibi Banda atakuwa wa kwanza kurudisha fomu yake Julai 24, akifuatiwa na Mutharika Julai 25. Chakwera atawasilisha fomu zake za uteuzi siku ya mwisho, Julai 30, wakati wagombea wengine watarudisha fomu zao ndani ya tarehe zilizopangwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma