

Lugha Nyingine
Rais wa Mauritania apongeza uhusiano imara na China, na kutazamia ushirikiano wa karibu zaidi
Rais wa Mauritania Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani akizungumza kwenye mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua na vyombo vingine vya habari vya China katika Ikulu ya Rais wa Mauritania mjini Nouakchott, Mauritania, Julai 17, 2025. (Xinhua/Han Xu)
NOUAKCHOTT - Rais Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani wa Mauritania amesema anajivunia sana urafiki imara na wa kudumu kati ya Mauritania na China na anatazamia ushirikiano mpana na wa kina zaidi wa pande mbili ambapo katika mahojiano ya hivi karibuni na Shirika la Habari la China, Xinhua na vyombo vingine vikuu vya habari vya China katika Ikulu ya Mauritania, Ghazouani ametoa pongezi za dhati juu ya maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Mauritania na China.
“Kwa msingi wa ushirikiano, mawasiliano ya kunufaishana na kuheshimiana kwa kutosha, uhusiano kati ya nchi hizo mbili unaendelea kuwa imra na wenye nguvu miongo sita iliyopita,” amesema, akirejelea uratibu muhimu wa pande mbili katika masuala ya kimataifa yanayofuatiliwa na pande zote mbili, ambayo mara nyingi yana ishara za misimamo sawa.
"Siku zote tunajitahidi kuendelea kuimarisha uhusiano huu kwa njia ambayo inatimiza matarajio ya watu wetu wa pande mbili wenye urafiki," ameongeza rais huyo.
Rais Ghazouani amesema kuwa tangu alipochaguliwa kuwa rais kwa mara ya kwanza mwaka 2019, ushirikiano kati ya Mauritania na China umeshuhudia maendeleo makubwa, ambayo yaliimarishwa wakati nchi hizo mbili zilipoinua uhusiano wao na kufikia ushirikiano wa kimkakati mwaka 2024.
Sasa ushirikiano wa pande mbili umepanuliwa ili kufikia maeneo kama vile miundombinu, uvuvi, afya, elimu, nishati, viwanda, usafiri na teknolojia ya kidijitali, na juhudi za mipango mipya ya maendeleo ambayo kupitia kwayo "tunategemea kuendeleza na kuufanya uchumi wa taifa kuwa wa sekta mbalimbali," ameongeza.
Akizungumzia kwa kusifu mikutano yake na Rais Xi Jinping wa China, Rais Ghazouani amesema katika mikutano hiyo, alihisi dhamira ya dhati na azma isiyochoka ya Rais Xi ya kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika kwa ujumla, na hasa Mauritania.
Ameongeza kuwa pia alihisi msisitizo mkubwa kutoka kwa Rais Xi juu ya nia ya China ya kuzisaidia nchi zenye maendeleo ya chini hasa zile za Afrika, kuzisaidia kuondokana na changamoto za kimaendeleo zinazowakabili, huku ikidumisha uhusiano wa uwazi unaozingatia kuheshimiana na maslahi ya pamoja.
Msisitizo huo, amesema, unaonyesha kwa kina sifa bora za uongozi zinazotambuliwa za Rais Xi na nia yake ya kuendeleza uhusiano wa China na nchi mbalimbali duniani ndani ya mfumo wa kuheshimiana na ushirikiano unaozingatia haki na usawa.
Akibainisha kuwa China ni mshirika mkuu wa kibiashara wa Mauritania, Ghazouani amesema biashara kati ya pande mbili imeshuhudia nguvu inayoongezeka ambapo mwaka 2024, thamani ya biashara kati ya nchi hizo mbili ilifikia dola za Kimarekani bilioni 2.42, ongezeko la asilimia 7.8 kuliko mwaka uliopita.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma