

Lugha Nyingine
China yasema inaunga mkono kwa uthabiti kazi ya UNESCO
BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Guo Jiakun amesema Jumatano kwenye mkutano na waandishi wa habari, China inaunga mkono kwa uthabiti kazi ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO).
Guo amesema China imeona kuwa UNESCO na nchi nyingi zimeelezea masikitiko yao juu ya uamuzi wa Marekani kujitoa tena kwenye shirika hilo.
"Ni mara ya tatu kwa Marekani kujitoa UNESCO, na nchi hiyo haijalipa ada ya mwanachama wa shirika hilo kwa muda mrefu. Hivi sivyo nchi kubwa inapaswa kufanya." Guo amesema.
"Nia ya Shirika la UNESCO ni kusukuma mbele ushirikiano wa kimataifa katika elimu, sayansi na utamaduni, kuhimiza maelewano na mafungamano kati ya nchi za ustaarabu mbalimbali, kulinda amani ya dunia, na kufikia maendeleo kwa pamoja,” amesema, akiongeza kuwa China inaunga mkono kwa uthaibti kazi ya UNESCO.
Msemaji huyo amesema, katika kuadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, China inatoa wito kwa nchi zote kusisitiza tena ahadi zao kwa ushirikiano wa pande nyingi, na kuchukua hatua madhubuti kuunga mkono mfumo wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa, kuunga mkono utaratibu wa kimataifa unaowekwa kwenye msingi wa sheria za kimataifa, na kuunga mkono kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa zinazowekwa kwenye msingi wa nia na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma