China yakabidhi mradi wa jengo la wodi ya wazazi nchini Cape Verde

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 24, 2025

Picha hii iliyopigwa tarehe 22 Julai 2025 ikionyesha mwonekano wa ndani wa jengo la wodi ya wazazi liliyojengwa na China katika Hospitali ya Dk. Baptista de Sousa mjini Mindelo, Kisiwa cha Sao Vincente, Cape Verde. (Kampuni ya 14 ya Kundi la Kampuni za Reli la China/kupitia Xinhua)

PRAIA, Cape Verde - Jengo la wodi ya wazazi lililojengwa kwa msaada wa China limekabidhiwa kwa Serikali ya Cape Verde mjini Mindelo, katika Kisiwa cha Sao Vincente ambapo Waziri Mkuu wa Cape Verde Ulisses Correia e Silva na Balozi wa China nchini humo Zhang Yang walihudhuria hafla ya makabidhiano siku ya Jumanne katika Hospitali ya Dk Baptista de Sousa.

Katika hotuba yake, Silva amesifu ushirikiano kati ya Cape Verde na China, akisema kuwa mradi huo ni mradi mkubwa zaidi wa miundombinu ya matibabu nchini Cape Verde tangu ipate uhuru.

Amelielezea jengo hilo jipya la wodi ya wazazi kuwa ni mafanikio makubwa ya ushirikiano wa kivitendo kati ya serikali hizo mbili, akisema litaboresha kwa kiasi kikubwa mfumo wa huduma ya afya ya mama na mtoto, kuongeza uwezo wa kimatibabu wa nchi nzima, na kuleta manufaa halisi kwa umma.

Silva ameelezea matumaini kuwa nchi hizo mbili zitaendelea kuongeza kwa kina uhusiano wao kiwenzi na kimkakati na kupanua ushirikiano katika maeneo zaidi.

Zhang, kwa upande wake, amesema mradi huo unawakilisha hatua nyingine muhimu katika urafiki na ushirikiano kati ya China na Cape Verde.

"Inaonyesha dhamira ya muda mrefu ya China ya kuunga mkono maendeleo ya afya ya Cape Verde na inaonyesha uhusiano wa kina kati ya watu wa nchi hizo mbili," amesema.

Zhang ameeleza nia ya China ya kuchukua makabidhiano hayo kama mwanzo mpya wa kusukuma mbele zaidi ushirikiano wa pande mbili katika sekta mbalimbali.

Likiwa limejengwa na Kampuni ya 14 ya Kundi la Kampuni za Reli la China, jengo hilo la wodi ya wazazi lina vitanda 150, vyumba vya kujifungulia vya kisasa, vyumba vya wagonjwa mahututi wa mambo ya uzazi, na vyumba vya upasuaji wa uzazi.

Mradi huo pia ni pamoja na msaada wa kiufundi wa miaka miwili, ambapo upande wa China utatoa mafunzo ya kitaaluma kwa wafanyakazi wa matibabu wa Cape Verde. 

Waziri Mkuu wa Cape Verde Ulisses Correia e Silva akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi jengo la wodi ya wazazi liliyojengwa na China katika Hospitali ya Dk. Baptista de Sousa mjini Mindelo, Kisiwa cha Sao Vincente, Cape Verde, Julai 22, 2025. (Kampuni ya 14 ya Kundi la Kampuni za Reli la China/kupitia Xinhua)

Balozi wa China nchini Cape Verde Zhang Yang akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi jengo la wodi ya wazazi liliyojengwa na China katika Hospitali ya Dk. Baptista de Sousa mjini Mindelo, Kisiwa cha Sao Vincente, Cape Verde, Julai 22, 2025. (Kampuni ya 14 ya Kundi la Kampuni za Reli la China/kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha