

Lugha Nyingine
Kenya yaongeza juhudi za kuchochea utalii wakati uhamaji mkubwa wa nyumbu ukianza
(CRI Online) Julai 25, 2025
Rais William Ruto wa Kenya amesema serikali itaimarisha kampeni kuongeza idadi ya watalii katika nchi hiyo.
Rais Ruto, ambaye amezindua matangazo ya kimataifa ya moja kwa moja mtandaoni ya Uhamaji Mkubwa wa Nyumbu mwaka 2025 katika Hifadhi ya Taifa ya Masai Mara, kusini magharibi mwa Kenya jana Alhamisi, amesema kampeni hiyo inalenga kuvutia watalii wa kigeni milioni 5 ifikapo mwaka 2027.
Kwa mujibu wa Wizara ya Utalii na Wanyamapori ya Kenya, idadi ya watalii wa kimataifa waliofika nchini Kenya iliongezeka kwa asilimia 15 na kufikia milioni 2.4 mwaka 2024, na mwaka jana mapato yaliyotokana na utalii yaliongezeka hadi dola bilioni 3.5 za kimarekani.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma