

Lugha Nyingine
Wataalamu wa Afrika wasema teknolojia ya Juncao inaweza kuboresha vyanzo vya kuongeza mapato na kilimo endelevu
Wataalamu wa kilimo wa Afrika wameeleza matazamio ya kutumiwa kwa teknolojia ya Juncao, ambayo ni teknolojia ya China inayotumika katika kilimo cha uyoga na chakula cha mifugo, kwa ajili ya kuboresha vyanzo vya kuongeza mapato katika jamii za vijijini kote barani Afrika.
Mkurugenzi mkuu wa bodi ya kilimo na raslimali za wanyama ya Rwanda Bw. Telesphore Ndabamenye, amesema teknolojia hiyo ina manufaa zaidi kwa kilimo cha uyoga, kwani ni uvumbuzi wa kina unaosaidia mazao, mifugo, ulinzi wa mazingira, lishe bora na uwezeshaji wa kiuchumi.
Akizungumza kwenye hafla ya kufunga warsha ya teknolojia ya Juncao mjini Kigali, mji mkuu wa Rwanda, Bw. Ndabamenye amesisitiza umuhimu wa teknolojia ya Juncao katika kuendeleza mageuzi ya kilimo, na matumizi yake mapana, hasa katika kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi zinazowakabili wakulima wadogo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma