

Lugha Nyingine
Afrika CDC yaonya kuhusu kuongezeka kwa usugu wa magonjwa dhidi ya dawa barani Afrika
(CRI Online) Julai 25, 2025
Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) kimeonya kuhusu kuongezeka kwa usugu wa magonjwa dhidi ya dawa barani Afrika, ikitishia kurudisha nyuma mafanikio ya miongo kadhaa ya afya na maendeleo.
Kwenye utafiti wake wa hivi karibuni kituo hicho kimesema kuna "kiwango cha kutisha" cha usugu wa bakteria dhidi ya dawa katika nchi 14 za Afrika na kuwa tishio la dharura ya afya ya umma.
Utafiti huo umechambua matokeo zaidi ya 187,000 ya vipimo kutoka maabara 205 kati ya mwaka 2016 na 2019 katika nchi 14, zikiwemo Ethiopia, Ghana, Kenya, Malawi, Mali na Nigeria, na kuleta matokeo yenye kuonesha kuongezeka kwa kutofanya kazi kwa dawa za kupambana na bakteria dhidi ya maambukizi ya kawaida ya bakteria.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma