Rais Xi Jinping apokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wapya nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 28, 2025

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba baada ya kupokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi 16 wapya nchini China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 25, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba baada ya kupokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi 16 wapya nchini China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 25, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi 16 wapya nchini China wakiwemo mabalozi wanne kutoka Afrika, ambao ni Dalva M. C. R. Allen wa Angola, Khaled Nazmy wa Misri, Franck E. W. Adjagba wa Benin na Morris Simon Batali wa Sudan Kusini ambapo akiwakaribisha wajumbe hao kwenye nyadhifa zao mpya, Rais Xi amewatakia wawafikishie salamu za heri viongozi na watu wa nchi zao, akielezea matumaini kuwa wajumbe hao watapata ufahamu wa pande zote na wa kina kuhusu China.

Mabalozi wengine waliokabidhi hati zao za utambulisho mjini Beijing siku ya Ijumaa ni: Pham Thanh Binh wa Vietnam, Miguel Lecaro Barcenas wa Panama, Jose Julio Gomez Beato wa Jamhuri ya Dominika, Riza Poda wa Albania, Jonathan Edward Austin wa New Zealand, Thaddeus Kambanei wa Papua New Guinea, Ramiro Jose Cruz Flores wa Nicaragua, Abdolreza Rahmani Fazli wa Iran, Pablo Arriaran wa Chile, Olexander Nechytaylo wa Ukraine, David Alfred Perdue Jr wa Marekani na Eliav Belotsercovsky wa Israel.

Rais Xi pia amekutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai Nurlan Yermekbayev.

Katika hotuba yake kwenye hafla hiyo, Rais Xi amesema kuwa China inathamini urafiki wake na watu duniani kote, na inapenda kuimarisha ushirikiano na mawasiliano ya pande zote na nchi nyingine kwa msingi wa kuheshimiana, usawa, kunufaishana.

Amesema kuwa, hivi sasa, China inasukuma mbele ustawishaji mkubwa wa taifa la China katika nyanja zote kupitia ujenzi wa mambo ya kisasa wa China, wakati huohuo uchumi wake ukidumisha mwelekeo tulivu wa kuimarika.

"China itashikilia kupanua ufunguaji mlango wa kiwango cha juu na kuwanufaisha watu wengi zaidi soko lake kubwa, ili maendeleo yake yalete fursa mpya kwa nchi nyingine na kuongeza uhakika mkubwa zaidi katika ukuaji wa uchumi wa dunia," Rais Xi amesema.

Amesema, huku kukiwa na kasi kubwa ya mabadiliko ya kimataifa na mazingira ya kimataifa yenye msukosuko, kuna haja kubwa kuliko wakati mwingine wowote kwa nchi duniani kote kuimarisha mshikamano na ushirikiano, kukumbatia maono mapana ya kuondokana na ufarakanishaji na migogoro, na kutilia maanani mustakabali wa binadamu wote.

"Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti, vilevile maadhimisho ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa," Rais Xi amesema.

Amesema China inapenda kushirikiana na nchi zote kulinda kithabiti mfumo wa kimataifa huku Umoja wa Mataifa ukiwa katika msingi wake na utaratibu wa kimataifa unaozingatia sheria za kimataifa.

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba baada ya kupokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi 16 wapya nchini China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 25, 2025. (Xinhua/Li Xiang)

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba baada ya kupokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi 16 wapya nchini China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 25, 2025. (Xinhua/Li Xiang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha