

Lugha Nyingine
Serikali ya China yapendekeza kuundwa kwa shirika la kimataifa la ushirikiano wa AI
SHANGHAI - Serikali ya China imependekeza kuundwa kwa shirika la ushirikiano wa kimataifa wa akili mnemba (AI), na inafikiria kuanzisha makao yake makuu mjini Shanghai, shirika la habari la China, Xinhua limefahamishwa kutoka vyanzo vya habari vinavyohusika na suala hilo.
Hii ni hatua muhimu ambayo China imefanya kutekeleza ushirikiano wa pande nyingi na kuhimiza mtindo wa usimamizi wa dunia ambao unahusisha kushauriana kwa pamoja, kujenga kwa pamoja na kunufaisha pamoja, vyanzo hivyo vimesema.
Pia vimeongeza kuwa ni hatua madhubuti iliyochukuliwa na China kuitikia wito wa Nchi za Kusini wa kuunganisha mgawanyiko wa kidijitali na akili mnemba, na kuhimiza maendeleo jumuishi ya AI na matumizi ya AI kwa manufaa.
China inatarajia shirika hilo litatumika kama jukwaa la nchi kuzidisha kwa kina ushirikiano katika uvumbuzi, kuhimiza ushirikiano wa kivitendo ili kufungua kikamilifu uwezo usio na kikomo wa AI, na kufikia maendeleo na ustawi wa pamoja.
Vimesema kupitia jukwaa hilo, China inatarajia kuzisaidia nchi za Kusini kuimarisha ujengaji wao wa uwezo, kukuza mazingira ya kimfumo ya uvumbuzi wa AI, kuhakikisha kuwa nchi zinazoendelea zinanufaika sawa na mawimbi ya AI, na kuhimiza utekelezaji wa Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya 2030 ya Maendeleo Endelevu.
Malengo zaidi ya shirika hilo, vyanzo hivyo vimesema, ni kuimarisha uratibu na uwiano wa mikakati ya maendeleo, sheria za usimamizi na viwango vya kiufundi miongoni mwa nchi, na kuunda hatua kwa hatua mfumokazi wa kimataifa na viwango vya kimataifa vya usimamizi wa AI ambavyo vina maafikiano mapana, kwa msingi wa kuheshimu kikamilifu tofauti za sera na utekelezaji miongoni mwa nchi.
Kwa kuanzisha makao makuu ya shirika hilo mjini Shanghai, China inatarajia kutumia kikamilifu faida yake bora katika AI - na faida bora ya Shanghai, hasa -- kukuza ushirikiano, vyanzo hivyo vya habari vimeeleza.
Vimesema kuwa China inapenda kujadili mipangilio husika na nchi ambazo zinapenda kujiunga na shirika hilo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma