Makubaliano ya ushuru kati ya EU na Marekani "hayaridhishi," "hayana uwiano": mbunge mwandamizi wa EU

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 28, 2025

Picha iliyopigwa Mei 23, 2025 ikionyesha bendera za Umoja wa Ulaya (EU) kwenye makao makuu ya Kamisheni ya Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

Picha iliyopigwa Mei 23, 2025 ikionyesha bendera za Umoja wa Ulaya (EU) kwenye makao makuu ya Kamisheni ya Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

BRUSSELS - Bernd Lange, mbunge mwandamizi wa Ulaya ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Ulaya juu ya Biashara ya Kimataifa amekosoa vikali mswada wa makubaliano ya kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya (EU) na Marekani, akionya kuwa unaweza kudhoofisha utulivu wa kiuchumi na usalama wa ajira wa umoja huo.

Lange, ameuelezea mfumokazi uliopendekezwa, ambao unahusu kutoza ushuru wa asilimia 15 kwa bidhaa zote za EU zinazouzwa kwa Marekani, kuwa "usioridhisha" na "usio na uwiano kwa kiasi kikubwa."

Amesema kuwa, kiwango hicho cha ushuru, kinawakilisha ongezeko mara nne zaidi ya viwango vya sasa vya wastani, wakati huohuo EU imeahidi ushuru sifuri kwa bidhaa za Marekani.

"Haya ni makubaliano yenye mwinamo. Kidhahiri, masharti ya makubaliano yamefanywa ambayo ni magumu kubeba," Lange amesema katika taarifa yake jana Jumapili.

Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Kamisheni ya EU Ursula von der Leyen walitangaza mapema jana Jumapili kwamba wamefikia makubaliano ya kibiashara ambapo Marekani itaweka ushuru wa asilimia 15 kwa bidhaa za EU.

Rais Donald Trump wa Marekani (Mbele) akihudhuria mkutano na waandishi wa habari kufuatia mkutano wa kilele wa NATO mjini  The Hague, Uholanzi, Juni 25, 2025. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

Rais Donald Trump wa Marekani (Mbele) akihudhuria mkutano na waandishi wa habari kufuatia mkutano wa kilele wa NATO mjini The Hague, Uholanzi, Juni 25, 2025. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

Ingawa viongozi wote wawili wameyaelezea makubaliano hayo kama hatua ya kurejesha "uwiano wa biashara" na kuhimiza biashara yenye usawa zaidi ya uelekeo wa pande mbili, makubaliano hayo yanaruhusu Washington kutoza ushuru mkubwa wakati huohuo ikipata ufikiaji wa ushuru-sifuri kwa bidhaa mbalimbali za kimkakati za Marekani kuuzwa nchi za nje.

Kinyume chake, EU imeahidi kununua nishati ya Marekani yenye thamani ya dola bilioni 750 na kuahidi kuwekeza dola za Kimarekani bilioni 600 nyingine nchini Marekani.

Lange amesema kuwa wakati Trump alitangaza hadharani ushuru wa jumla wa asilimia 15 katika hotuba kufuatia mazungumzo ya makubaliano hayo, hapo awali alikuwa ameziondoa sekta fulani, zikiwemo za chuma na dawa.

Ameongeza kuwa Ulaya inatarajiwa kuongeza kununua nishati ya Marekani, hasa gesi ya kimiminika, kwani EU inaendelea na jitihada za kupunguza utegemezi wake kwa nishati ya mafuta ya Russia.

Hata hivyo, Lange amekosoa uwekezaji mwingine wa dola bilioni 600 uliopangwa, ikiwemo kuongezeka ufadhili kwa teknolojia ya kijeshi ya Marekani, akielezea hatua kama hizo ni kinyume na maslahi ya kiuchumi ya Ulaya.

Mteja akilipa kwenye supamaketi mjini Brussels, Ubelgiji, Aprili 1, 2022. (Xinhua/Zheng Huansong)

Mteja akilipa kwenye supamaketi mjini Brussels, Ubelgiji, Aprili 1, 2022. (Xinhua/Zheng Huansong)

"Kwa ujumla, makubaliano haya yatatoa mchango katika kudhoofisha maendeleo ya kiuchumi ya EU na kudhuru pato lake la jumla," amesema. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha