AU yakaribisha Ufaransa kutambua Nchi ya Palestina

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 28, 2025

Picha hii iliyopigwa Februari 13, 2025 ikionyesha majengo ya Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU)  huko Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia. (Xinhua/Michael Tewelde)

Picha hii iliyopigwa Februari 13, 2025 ikionyesha majengo ya Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) huko Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia. (Xinhua/Michael Tewelde)

ADDIS ABABA - Umoja wa Afrika (AU) umekaribisha Ufaransa kutangaza kuitambua rasmi Nchi ya Palestina, ukilieleza kuwa ni "hatua muhimu" inayolinga na msimamo wa muda mrefu wa AU.

Katika taarifa iliyotolewa Jumamosi, Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU Mahmoud Ali Youssouf amesema tangazo hilo la Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, lililoelezea nia yake ya kuitambua Nchi ya Palestina, "linaligana na msimamo wa muda mrefu wa Umoja wa Afrika."

Youssouf amesema msimamo huo ulisisitizwa hivi karibuni wakati wa Mkutano wa 38 wa Kawaida wa Baraza Kuu la AU. Amesema mkutano huo, ambao ulihudhuriwa na wakuu wa nchi na serikali za Afrika kwenye makao makuu ya AU katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa mwezi Februari mwaka huu, ulisisitiza "ahadi ya pamoja ya Afrika kwa haki isiyonyimika ya watu wa Palestina, ikiwemo haki yao ya kujitawala na kuanzisha nchi yao."

Wajumbe wa ujumbe wa Palestina wakishiriki kwenye  hafla ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, Ufaransa, Julai 26, 2024. (Picha na Wang Dongzhen/POOL/Xinhua)

Wajumbe wa ujumbe wa Palestina wakishiriki kwenye hafla ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, Ufaransa, Julai 26, 2024. (Picha na Wang Dongzhen/POOL/Xinhua)

Mwenyekiti wa chombo hicho cha bara la Afrika kilichoundwa na nchi wanachama 55 amesema taarifa ya Ufaransa ni "hatua muhimu kuelekea utatuzi wa haki, wa kudumu na kwa pande zote wa mgogoro kati ya Israel na Palestina kwenye msingi wa sheria za kimataifa na maazimio husika ya Umoja wa Mataifa."

Youssouf pia amesisitiza "uungaji mkono usioyumba" wa AU kwa mpango wa nchi mbili, huku Israeli na Palestina zikiishi pamoja kwa amani na usalama. Aidha amehimiza nchi nyingine kuiga mfano huo katika kuunga mkono "matarajio halali ya watu wa Palestina."

Alhamisi wiki iliyopita, Rais Macron alitangaza kwamba Ufaransa itaitaitambua rasmi Nchi ya Palestina wakati wa mkutano ujao wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Septemba. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha