Timu za matibabu za China zazindua kampeni ya elimu ya afya na kliniki bila malipo visiwani Zanzibar

(CRI Online) Julai 28, 2025

Timu ya mradi wa kudhibiti ugonjwa wa kichocho ya China na kundi la 34 la timu ya madaktari wa China visiwani Zanzibar, Tanzania Jumamosi walizindua kampeni ya elimu ya afya na kliniki bila malipo visiwani humo.

Kiongozi wa timu hiyo ya mradi wa kudhibiti kichocho Dai Yang, amesema kampeni hiyo ilizinduliwa wakati ambapo kuna msimu wa mvua wa muda mrefu ambao umesababisha ongezeko la maambukizi yanayotokana na maji na matukio ya majeraha.

Amebainisha kuwa mvua kubwa imesababisha mafuriko na uharibifu mkubwa wa barabara, ikileta mazingira mazuri ya kuzaliana kwa wingi kwa konokono wa Biomphalaria, ambao ni wabebaji wa awali wa vimelea vya kichocho, huku ufikiaji huduma za matibabu ukitatizika sana, ikiwaacha wakazi wengi bila kutibiwa majeraha na maambukizi.

Ikitambua hatari ya watoto kucheza kwenye maji yaliyotuama, timu hiyo ya mradi wa kudhibiti kichocho imeweka mkazo maalum katika kuelimisha wanafunzi huku timu ya matibabu ya China pia ilitoa ushauri na matibabu bila malipo kwa mamia ya wakazi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha