

Lugha Nyingine
Wakazi zaidi ya 50 wa Zanzibar wapata uoni tena katika kampeni ya upasuaji mtoto wa jicho iliyoongozwa na madaktari wa China
Wakazi zaidi ya 50 wa Zanzibar wamerejesha uwezo wao wa kuona kufuatia kampeni ya wiki moja ya upasuaji mtoto wa jicho iliyofanywa na Kundi la 34 la timu ya madaktari wa China visiwani Zanzibar, Tanzania.
Ikiongozwa na daktari wa macho Zhou Shi, timu hiyo ilifanya upasuaji wa mtoto wa jicho kwa wagonjwa zaidi ya 50 kuanzia Julai 21 hadi 25 licha ya vifaa vichache, vizuizi vya lugha na changamoto za ndani za upasuaji.
Ahmed Muumin, mkurugenzi wa magonjwa ya macho katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, amepongeza kampeni hiyo akisema madaktari wa China wamesaidia kupanda mbegu za 'mwanga' visiwani Zanzibar.
Naye kiongozi wa timu hiyo ya madaktari wa China, Chen Wei, amebainisha kuwa kampeni hiyo ni sehemu muhimu ya mpango wa maendeleo ya matibabu wa China-Zanzibar wa 2025.
Tangu mwaka 1964, timu za madaktari wa China zimetibu mamilioni ya watu kote Zanzibar, na kuwarejesha uwezo wa kuona maelfu ya watu na kuimarisha uhusiano wa kibinadamu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma