

Lugha Nyingine
Tamasha la “Giants of Africa” laanza nchini Rwanda likichanganya michezo, utamaduni na uongozi
(Picha/Xinhua)
Tamasha la “Giants of Africa” la mwaka 2025 limeanza mjini Kigali, nchini Rwanda, siku ya Jumamosi, likiwaleta pamoja vijana na makocha wapatao 400 kutoka kote barani Afrika katika shamrashamra za wiki nzima zinazohusisha mpira wa kikapu, utamaduni, muziki, elimu na uhusiano.
Tamasha hilo linalofanyika chini ya kaulimbiu ya "Afrika Isiyo na Mipaka," linalenga kutumia nguvu ya ushawishi wa michezo ili kuelimisha, kuhamasisha, na kuwezesha viongozi wa kizazi kijacho wa Afrika, huku likihimiza umoja na fursa za kuvuka mipaka.
Mbali na ushiriki wa vijana, tukio hilo pia huwaleta pamoja washauri kutoka kote Afrika na kwingineko, likiunda jukwaa lenye hamasa kwa ajili ya mabadilishano ya ujuzi na ukuaji.
Tamasha hilo limepangwa kuendelea hadi Agosti 2.
(Picha/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma