Raia takriban 43 wauawa katika shambulizi linaloshukiwa kufanywa na waasi wa ADF mashariki mwa DRC

(CRI Online) Julai 28, 2025

Vyanzo vya habari ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) vimeripoti kuwa takriban raia 43 wameuawa usiku wa Jumamosi kuamkia jana Jumapili katika shambulizi linaloshukiwa kufanywa na waasi wa kundi la Allied Democratic Forces (ADF) katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Vyanzo hivyo vimeeleza, wapiganaji wa ADF walivamia kanisa la Kikatoliki mapema Jumamosi katika mji wa Komanda, Jimbo la Ituri.

Kiongozi wa jumuiya ya kiraia katika eneo la Komanda amesema wengi wa waliofariki, hasa waumini wa Kikatoliki walikuwa wakijiandaa kwa sherehe za Jumapili wakati shambulizi hilo lilipotokea.

Amesema, nyumba kadhaa zimechomwa moto, na idadi isiyojulikana ya watu bado hawajulikani walipo.

Mashuhuda wamesema kuwa washambuliaji hao pia wamepora benki ya eneo hilo na mali nyingine za jumuiya kabla ya kukimbilia kwenye msitu wa karibu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha