Rais Xi ahimiza kufanya juhudi kwa nguvu zote kulinda maisha ya watu wakati wa mafuriko

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 29, 2025

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amehimiza kufanya juhudi kwa nguvu zote kuhakikisha usalama wa maisha na mali za watu katika kupambana na mafuriko na majanga ya kijiolojia yanayosababishwa na mvua kubwa zinazoathiri baadhi ya maeneo ya China kwa hivi sasa.

Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametoa maagizo muhimu kuhusu kudhibiti mafuriko na kutoa msaada.

Rais Xi amesema, ni lazima kufanya juhudi kwa nguvu zote za kutafuta na kuokoa watu wasiojulikana walipo au wamenaswa, na kuwahamisha mara moja wakaazi katika maeneo yanayotishiwa na mafuriko na kuwapangia makazi mengine ili kupunguza vifo na majeruhi.

Pia amehimiza idara zote husika kupanga mipango ya kukabiliana na hali mbaya na mazingira mabaya zaidi, kutekeleza kihalisi wajibu wa kisiasa, kutekeleza kwa makini zaidi hatua mbalimbali za kudhibiti mafuriko, kufuatilia zaidi sehemu zenye hali dhaifu na kuweka mkazo katika maeneo muhimu, na kugawa waokoaji na zana na vifaa kwa njia ya kisayansi.

"Ni lazima kukabiliana na hali ya dharura mapema iwezekanavyo, na kutoa nguvu zote kwa kulinda maisha na mali za watu," amesema.

Hivi karibuni, mvua kubwa mfululizo zimenyesha katika maeneo ya mashariki, kaskazini na kaskazini mashariki mwa China, zikileta mafuriko na majanga ya kijiolojia na kusababisha maafa makubwa katika miji na mikoa ya Beijing, Hebei, Jilin na Shandong.

Katika maagizo yake, Waziri Mkuu wa China Li Qiang amehimiza idara ya kitaifa ya udhibiti wa mafuriko kusaidia serikali za mitaa kuimarisha kazi ya kukabiliana na maafa ya mvua kubwa na mafuriko.

Li, ambaye pia ni mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, ametoa agizo la kufanya vizuri ufuatiliaji wa hali ya hewa iliyokithiri, kuimarisha ukaguzi wa hali ya ukingo wa mito na mabwawa ya maji, ili kugundua mapema hatari za mafuriko katika maeneo ya mijini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha