

Lugha Nyingine
Zaidi ya watu milioni 88 wakumbwa na baa la njaa katika maeneo ya Afrika Mashariki na Kati
Taarifa ya pamoja iliyotolewa Jumatatu na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Mamlaka ya Kiserikali kwa Maendeleo ya Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) inaonyesha kuwa hadi mwishoni mwa mwezi Juni mwaka 2025, watu takriban milioni 88.5 katika eneo la Afrika Mashariki na Kati wanakumbwa na ukosefu mkubwa wa usalama wa chakula na kuhitaji haraka msaada wa kibinadamu.
Kwenye taarifa mpya ya Juni kuhusu hali ya usalama wa chakula na lishe, FAO na IGAD zimesema kati ya watu hao wanaokumbwa na baa la njaa, milioni 57.1 wako katika nchi saba kati ya nchi nane wanachama wa IGAD, ambazo ni Djibouti, Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, na Uganda.
"Kiwango cha ukosefu mkubwa wa usalama wa chakula kwenye eneo zima bado kinaendelea kuleta wasiwasi, huku misimu ya upungufu wa chakula inayoendelea au inayokaribia ikizidisha athari za vurugu, mishtuko ya tabianchi na changamoto za kiuchumi kwenye nchi nyingi” mashirika hayo yamesema.
Mashirika hayo yameeleza kuwa, nchi zenye migogoro na zenye ukosefu wa usalama ndizo zimeathiriwa vibaya zaidi, kwa kuwa msukosuko huo unaendelea kusumbua maisha ya watu na kudhoofisha usalama wa chakula kwenye eneo hilo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma