Askari wawili wafariki katika ajali ya ndege ya jeshi kaskazini mwa Morocco

(CRI Online) Julai 29, 2025

Wanajeshi wawili wamefariki jana Jumatatu asubuhi baada ya ndege ya mafunzo ya kijeshi aina ya Alpha inayomilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Morocco (FAR) kuanguka kaskazini mwa nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na FAR imesema, ajali hiyo imetokea katika Uwanja wa Ndege wa Fez-Saiss mjini Fez wakati wa mafunzo, ambapo ndege hiyo ilipoteza mwelekeo na kuanguka katika njia ya kuruka ndege wakati ikijiandaa kuruka.

Taarifa hiyo pia imesema, mamlaka za usalama zimeanza uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha