

Lugha Nyingine
Baraza la Usalama la UN larefusha muda wa vikwazo dhidi ya makundi yenye silaha nchini CAR
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) limepitisha azimio jana Jumanne kurefusha kwa mwaka mmoja hadi tarehe 31 Julai mwaka 2026, muda wa vikwazo dhidi ya makundi yenye silaha nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) vilevile watu wengine ambao wanadhoofisha amani nchini humo.
Likiwa limepitishwa kwa kauli moja na nchi zote wanachama 15 wa baraza hilo, azimio hilo namba 2789 linazielekeza nchi wanachama wote “kuchukua hatua za lazima ili kuzuia usambazaji, uuzaji na uhamishaji wa moja kwa moja kwa njia isiyo ya moja kwa moja wa silaha au vifaa husika vya aina zote kwa makundi yenye silaha na watu binafsi wenye uhusiano nayo wanaofanya operesheni nchini humo.”
Mbali na hayo, azimio hilo pia linarefusha muda wa jukumu la jopo la wataalamu wanaosaidia utekelezaji wa vikwazo hivyo hadi tarehe 31 Agosti mwaka 2026.
Mandhari ya Kipekee ya Karst katika Mkoa wa Guizhou yavutia watalii
Tamasha la kimataifa la densi lafunguliwa katika Mkoa wa Xinjiang, China likiwa na maonyesho 52
Wakulima wa China wawa na pilikapilika za uzalishaji wa kilimo katika kipindi cha Dashu
Maliasili nyingi za chumvi zaongeza mapato ya wanakijiji katika Wilaya ya Gegye, Xizang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma