Mjumbe wa China asema, Mazungumzo ya kibiashara kati ya China na Marekani ni ya kina, ya wazi na ya kiujenzi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 30, 2025

Li Chenggang, mjumbe wa biashara ya kimataifa wa China katika Wizara ya Biashara ya China na naibu waziri wa biashara wa China akiongea na waandishi wa habari baada ya duru mpya ya mazungumzo ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani mjini Stockholm, Sweden, Julai 29, 2025. (Xinhua/Peng Ziyang)

STOCKHOLM - Timu za kibiashara na kiuchumi za China na Marekani zimefanya mazungumzo ya kina, ya wazi na ya kiujenzi juu ya mada muhimu za maslahi yanayofuatiliwa na pande zote, Li Chenggang, mjumbe wa biashara ya kimataifa wa China katika Wizara ya Biashara ya China amesema mjini Stockholm jana Jumanne wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya duru mpya ya mazungumzo ya kiuchumi na kibiashara katika mji mkuu huo wa Sweden.

"Pande hizo mbili zitaendelea kuhimiza Marekani kuongeza muda wa kusimamisha kutoza ushuru wa asilimia 24 wa kulipizana sawa, vilevile hatua za kulipiza za China," amesema Li ambaye pia ni naibu waziri wa biashara wa China.

"Pande zote mbili zinafahamu kikamilifu umuhimu wa kulinda uhusiano tulivu na mzuri wa kiuchumi kati ya China na Marekani," Li amesema, akiongeza kuwa pande hizo mbili zimefanya mazungumzo ya wazi juu ya masuala makubwa ya kibiashara na kiuchumi yanayofuatiliwa na kila mmoja.

Amesema katika kipindi cha siku moja na nusu iliyopita, pande hizo mbili zilifanya majumuisho ya hali ya utekelezwaji wa maafikiano ya Geneva na London na kutambua kwa kutosha maendeleo yaliyopatikana.

"Timu za kiuchumi na kibiashara za China na Marekani zitadumisha mawasiliano ya karibu, kufanya kwa wakati mazungumzo juu ya masuala ya kibiashara na kiuchumi, na kuendelea kuhimiza maendeleo tulivu na mazuri ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili," Li amesema. 

Li Chenggang, mjumbe wa biashara ya kimataifa wa China katika Wizara ya Biashara ya China na naibu waziri wa biashara wa China akiongea na waandishi wa habari baada ya duru mpya ya mazungumzo ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani mjini Stockholm, Sweden, Julai 29, 2025. (Xinhua/Peng Ziyang)

Li Chenggang, mjumbe wa biashara ya kimataifa wa China katika Wizara ya Biashara ya China na naibu waziri wa biashara wa China akiongea na waandishi wa habari baada ya duru mpya ya mazungumzo ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani mjini Stockholm, Sweden, Julai 29, 2025. (Xinhua/Peng Ziyang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha