Jeshi la Thailand ladai Cambodia kukiuka makubaliano ya kusimamisha vita, Cambodia yasema mgogoro wa mpaka umeisha

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 30, 2025

Picha hii iliyopigwa Julai 28, 2025 ikionyesha nyumba iliyobomolewa baada ya kushambuliwa na makombora katika Jimbo la Oddar Meanchey, Cambodia. (Picha na Nitola/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Julai 28, 2025 ikionyesha nyumba iliyobomolewa baada ya kushambuliwa na makombora katika Jimbo la Oddar Meanchey, Cambodia. (Picha na Nitola/Xinhua)

BANGKOK/PHNOM PENH - Jeshi la Thailand limesema Jumanne kwamba Cambodia imekiuka makubaliano ya kusimamisha vita, lakini Thailand bado inafanya kazi kuwezesha mazungumzo kati ya makamanda wa pande zote mbili walioko mstari wa mbele, ambayo yalikuwa yameahirishwa hadi saa 4 asubuhi kwa saa za huko.

Siku hiyo hiyo, Naibu Katibu Mkuu ambaye pia ni msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Cambodia, Luteni Jenerali Maly Socheata alisema mapigano ya silaha kati ya wanajeshi wa Cambodia na Thailand katika maeneo ya mpaka yenye mgogoro yamemalizika.

Winthai Suvaree, msemaji wa Jeshi la Thailand, mapema Jumanne asubuhi alitoa taarifa, akisema kwamba Thailand imetekeleza usimamishaji vita mara moja kwenye mpaka kati ya Thailand na Cambodia mara tu baada ya makubaliano ya kusimamisha vita kuanza kutekelezwa.

"Hata hivyo, inasikitisha kwamba wakati muda wa mwisho wa kusimamisha vita ulipofika, Thailand imebaini Cambodia ikifanya mashambulizi ya silaha katika maeneo mengi ndani ya mipaka ya Thailand," imesema taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa tangazo la awali la Jeshi la Thailand, baada ya kusimamisha vita kuanzia usiku wa manane siku ya Jumatatu, eneo moja kwenye mpaka lilisumbuliwa na Cambodia, ikisababisha kushambuliana kwa silaha kulikoendelea hadi jana Jumanne asubuhi. Aidha, limeeleza kuwa mapigano pia yalitokea katika eneo lingine na kuendelea hadi saa 11:30 alfajiri kwa saa za huko jana Jumanne.

Mapema Jumanne, Jeshi la Thailand lilithibitisha kupitia mitandao ya kijamii kwamba usimamishaji vita umetekelezwa katika maeneo yote ya mpaka kati ya Thailand na Cambodia.

"Mapigano ya silaha kati ya wanajeshi wa Cambodia na Thailand katika maeneo ya mpaka yenye mgogoro yamemalizika baada ya viongozi wa nchi hizo mbili kukubaliana kusimamisha vita," Socheata amesema Jumanne.

Naye Waziri Mkuu wa Cambodia Hun Manet alisema mapema Jumanne asubuhi kuwa, hali ya mpaka kati ya Cambodia na Thailand imetulia baada ya usimamishaji vita kuanza kutekelezwa kuanzia saa sita usiku siku ya Jumatatu.

Viongozi wa Thailand na Cambodia wamekubaliana kutekeleza usimamishaji vita kuanzia usiku wa manane juzi Jumatatu, Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim alisema baada ya mkutano wa Jumatatu ulioandaliwa naye nchini Malaysia. 

Picha hii iliyopigwa Julai 28, 2025 ikionyesha nyumba iliyobomolewa baada ya kushambuliwa na makombora katika Jimbo la Oddar Meanchey, Cambodia. (Picha na Nitola/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Julai 28, 2025 ikionyesha nyumba iliyobomolewa baada ya kushambuliwa na makombora katika Jimbo la Oddar Meanchey, Cambodia. (Picha na Nitola/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Julai 28, 2025 ikionyesha nyumba iliyobomolewa baada ya kushambuliwa na makombora katika Jimbo la Oddar Meanchey, Cambodia. (Picha na Nitola/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Julai 28, 2025 ikionyesha nyumba iliyobomolewa baada ya kushambuliwa na makombora katika Jimbo la Oddar Meanchey, Cambodia. (Picha na Nitola/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha