Afrika Kusini yasema kazi ya kufikia makubaliano ya ushuru na Marekani inaendelea

(CRI Online) Julai 30, 2025

Wizara ya Biashara, Viwanda na Ushindani ya Afrika Kusini imesema katika taarifa yake Jumanne, kwamba nchi hiyo inajitahidi kufikia makubaliano na Marekani, huku ushuru wa asilimia 30 uliowekwa na Washington kwa Afrika Kusini ukianza kutozwa rasmi baada ya siku tatu zijazo.

Wizara hiyo imesema wanaendelea kudhamiria kwa jambo hilo wakati wanaposubiri maoni ya dhati kutoka kwa wenzao wa Marekani kuhusu hatma ya makubaliano yao ya utaratibu.

Imebainisha zaidi kuwa mazungumzo mfululizo yamekuwa yakiendelea na Marekani, na kwamba wamesaini hati ya utangulizi wa masharti na kujiandaa kwa ajili ya kuingia kwenye makubaliano, ambayo yatafuata mwelekeo wa Marekani.

Pia imekanusha mpango wowote wa "kujitenganisha" na Marekani, ikibainisha kuwa Afrika Kusini "imechukua uamuzi wa kutolipiza kisasi" kwa ushuru uliotangazwa na Washington.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha