Rais wa Rwanda asema yuko tayari kuimarisha ushirikiano na China

(CRI Online) Julai 30, 2025

Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema China ni rafiki mwema, na anatazamia kuimarisha urafiki wa jadi na ushirikiano wa kivitendo kati ya nchi hizo mbili.

Rais Kagame ametoa kauli hiyo jana Jumanne alipokuwa akipokea hati ya utambulisho ya balozi mpya wa China nchini humo Bw. Gao Wenqi.

Rais huyo amesema serikali na watu wa Rwanda watatoa uungaji mkono kamili na uwezeshaji kwa balozi Gao kutekeleza kazi zake.

Kwa upande wake Balozi Gao amebainisha kuwa chini ya mwongozo wa kimkakati wa marais wa nchi hizo mbili, uhusiano kati ya China na Rwanda umeinuliwa na kuwa ushirikiano wa washirika wa kimkakati wa pande zote ukijumuisha matunda katika sekta zote.

Ameongeza kuwa China iko tayari kufanya kazi na Rwanda ili kuongeza kuaminiana kisiasa na kuhimiza ushirikiano wa kivitendo ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi zote mbili.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha