Wabunge wa Rwanda waidhinisha makubaliano ya amani na DRC ili kuimarisha utulivu wa kikanda

(CRI Online) Julai 31, 2025

Baraza la chini la Bunge la Rwanda limepitisha kwa kauli moja jana Jumanne sheria inayoidhinisha makubaliano ya amani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ikilenga kurejesha amani na usalama katika Eneo la Maziwa Makuu.

Makubaliano hayo yaliyosainiwa tarehe 27 Juni mjini Washington, D.C. na kuungwa mkono na wabunge wote 76 waliopo, yanalenga kutafuta ufumbuzi wa mivutano na changamoto za kiusalama za muda mrefu kati ya nchi hizo mbili.

Kwenye mjadala wa bunge kuhusu makubaliano hayo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda Olivier Nduhungirehe amesema, makubaliano hayo yalisainiwa nchini Marekani, ambayo ilishiriki katika mchakato huo, chini ya upatanishi wa Qatar na uungaji mkono wa Umoja wa Afrika.

“Hii ni hatua muhimu kuelekea kurejesha amani, usalama na kuaminiana kati ya Rwanda na DRC” Nduhungirehe amewaambia wabunge.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha