Waziri wa Ulinzi wa China asisitiza tena Jeshi la China liko tayari kwa muungano wa taifa kwenye hafla ya Siku ya Jeshi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 01, 2025

BEIJING - Waziri wa Ulinzi wa China Dong Jun amesema kuwa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) liko tayari wakati wote kwa ajili ya muungano kamili wa taifa la China, kamwe kutoruhusu majaribio yoyote ya mafarakano ya "kuifanya Taiwan ijitenge" na kuzuia wakati wote uingiliaji wowote wa kijeshi kutoka nje.

Dong amesema hayo jana Tarehe 31 Julai kwenye tafrija kubwa iliyoandaliwa na Wizara ya Ulinzi wa Taifa ya China mjini Beijing, kwa kuadhimisha siku ya Tarehe Mosi Agosti ambayo ni siku ya miaka 98 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA).

“Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Wajapan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti, na pia ni maadhimisho ya miaka 80 tangu kurejeshwa kwa Taiwan na mwaka wa 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa,” Dong amesema.

Tarehe 3 Septemba, China itafanya gwaride la kijeshi kwenye Uwanja wa Tian'anmen mjini Beijing kusherehekea maadhimisho ya ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Wajapan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti.

Dong amesema gwaride hilo litadhihirisha kwa Chama na watu wa China kwamba Jeshi la Ukombozi wa Umma la China ni nguvu inayolinda amani na haki, na ina nguvu bora halisi ya kijeshi.

Pia amesema kuwa jeshi hilo la China linapenda kushirikiana na wenzao wa nchi mbalimbali duniani katika kutimiza matumaini ya jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja na mapendekezo makuu matatu ya Dunia, kukabiliana na hatari na changamoto, na kujenga dunia yenye amani ya kudumu, usalama kwa wote, ustawi kwa pamoja, uwazi na ujumuishwaji, na yenye mazingira safi na ya kupendeza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha