Miujiza ya Wanyamapori: Kutoka Mbuga Tambarare za Afrika hadi Uwanda wa Juu wa Qinghai -Tibet, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 30, 2025
Miujiza ya Wanyamapori: Kutoka Mbuga Tambarare za Afrika hadi Uwanda wa Juu wa Qinghai -Tibet, China
Twiga akitembea kupita karibu na kundi la nyumbu katika Hifadhi ya Kitaifa ya Masai Mara nchini Kenya.

Katika wakati wa majira ya joto mwaka huu, ukataji tiketi kwa safari za kimataifa nchini China umeongezeka kwa karibu 50%, kuliko mwaka jana huku safari za kwenda Afrika zimeongezeka kwa asilimia takriban 103 kuliko mwaka jana. Kushuhudia uhamaji mkubwa wa wanyamapori katika Afrika Mashariki kumekuwa mvuto mkubwa kwa watalii wa China.

Kuanzia kila mwezi wa Julai, mamilioni ya nyumbu, pundamilia, na wanyamapori wengine huanza safari yenye hatari. Wakisukumwa na utafutaji maji na nyasi mbichi, huhama kutoka Mbuga ya Kitaifa ya Serengeti ya Tanzania kuelekea kaskazini hadi Hifadhi ya Kitaifa ya Masai Mara ya Kenya.

Hifadhi hizi mbili zimeunda mfumo mkubwa wa ikolojia wa Mara-Serengeti. Kuanzia Julai hadi Septemba, msimu wa kiangazi kusini mwa Serengeti husukuma mifugo kuelekea malisho ya kijani ya Masai Mara kaskazini.

Kuvuka Mto Mara kunahusisha uvukaji wa kufa na kupona, kutokana na kuwepo kwa matishio kutoka kwa mamba wanaonyemelea na hatari ya kuzama. Hata wanapofika ng'ambo ya pili, wanyama wawindaji wengine kama simba na fisi huwangoja wanyama hao waliochoka.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha