Spika wa Bunge la Umma la China afanya ziara rasmi nchini Uswisi

(CRI Online) Agosti 01, 2025

Spika wa Bunge la Umma la China Zhao Leji amefanya ziara rasmi nchini Uswisi kuanzia tarehe 28 hadi 31 mwezi uliopita, ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Baraza la Taifa la Bunge la Uswisi Maja Riniker.

Katika mazungumzo hayo, Spika Riniker amesema kwa kufuata msingi wa kuheshimiana na kufungua mlango, uhusiano kati ya Uswisi na China umeendelea kwa utulivu, na kupata mafanikio makubwa.

Naye Spika Zhao amesema katika miaka 75 iliyopita tangu China na Uswisi kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia, nchi hizo mbili zimekuza moyo wa ushirikiano wa “Usawa, Uvumbuzi na Mafanikio ya pamoja”, na kuwa mfano mzuri kati ya nchi zenye mifumo tofauti, ukubwa tofauti, na viwango tofauti vya maendeleo.

Ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na Uswisi, ili kuhimiza uhusiano wao wa washirika wa kimkakati wa kiuvumbizi kuwa na kiwango cha juu zaidi.

Spika Zhao pia amefanya mazungumzo na Rais wa Baraza la Muungano la Uswisi Andrea Caroni.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha