Idadi ya watalii wanaotembelea Kenya yaongezeka kwa asilimia 2.3 katika miezi mitano ya mwaka 2025

(CRI Online) Agosti 01, 2025

Idara ya Takwimu ya Taifa ya Kenya (KNBS) imetoa ripoti jana Alhamisi ikisema idadi ya watalii wanaokuja Kenya imeongezeka kwa asilimia 2.3 katika miezi mitano ya mwanzo ya mwaka 2025, hali ambayo inatokana na jitihada za Kenya kuleta uanuwai kwenye bidhaa za utalii na masoko ya utalii.

Ripoti hiyo imesema katika kipindi hicho Kenya imepokea watalii 922,961, ikilinganishwa na watalii 902,076 wa mwaka 2024 wakati kama huu.

Kwa mujibu wa takwimu za KNBS, idadi ya watalii ya mwezi Januari ilikuwa kubwa zaidi ikifikia watalii 217,753, ikifuatiwa na watalii 196,146 wa Februari na 171,269 wa Machi.

Aidha, imeeleza kuwa, watalii wengi zaidi waliingia Kenya kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha